MAULIDI SINGIDA YAJAA BARAKA NA DUA KWA TAIFA
Автор: CALES TV
Загружено: 2025-10-21
Просмотров: 48
Описание:
SINGIDA
Waumini wa dini ya Kiislamu katika Manispaa ya Singida wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika maulidi maalum yaliyofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya zamani, ambapo pamoja na kusherehekea tukio hilo tukufu, walifanya swala maalum ya kuliombea Taifa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mgeni rasmi katika maulidi hayo alikuwa Mkuu wa Taasisi ya Said Shohadaa Foundation Kanda ya Afrika, yenye makao makuu yake jijini Arusha, Sheikh Maulid Sombi, ambaye pia aliongoza swala hiyo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni kutoka nchi jirani ya Kenya pamoja na mikoa mbalimbali nchini, ikiwa ni ishara ya umoja na mshikamano wa waumini wa Kiislamu katika kuombea amani, upendo na ustawi wa Taifa.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: