SHEIKH NASSOR: “AMANI HAIJENGWI KWA UMWAGAJI WA DAMU”
Автор: CALES TV
Загружено: 2025-11-09
Просмотров: 217
Описание:
Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Singida wametakiwa kuepuka kujihusisha na vurugu au maandiko yanayosambazwa mitandaoni yanayoweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.
Wito huo umetolewa na Sheikh wa Mkoa wa Singida, Alhaji Issa Nassor, wakati akizungumza na waumini wa dini hiyo katika msikiti wa Wilaya ya Ikungi hivi karibuni.
Sheikh Nassor amesema kuwa baadhi ya watu, hasa kupitia mitandao ya kijamii na wanaharakati wasio na imani wala heshima kwa mamlaka za nchi, wamekuwa wakieneza ujumbe unaoweza kuchochea vurugu, jambo ambalo ni kinyume na mafundisho ya dini.
“Amani ya nchi yetu imejengwa kwa maridhiano na siyo kwa umwagaji wa damu. Hata Mtume Muhammad (S.A.W) alikomboa mji wa Makka kwa amani na mazungumzo,” alisema Sheikh Nassor.
Aidha, amesema vitabu vya dini vinaelekeza wafuasi wote kutii mamlaka zilizowekwa, kwa kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya imani na utiifu kwa Mwenyezi Mungu.
Sheikh Nassor amewataka viongozi wa dini na wazazi kuhakikisha wanawaelimisha vijana juu ya umuhimu wa kulinda amani na kuepuka ushawishi wa watu wanaotumia mitandao kwa nia ya kuleta migawanyiko.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: