INADES NA JUKWAA LA USTAWI WA PUNDA WABADILI MTAZAMO WA JAMII KUHUSU PUNDA
Автор: CALES TV
Загружено: 2025-08-02
Просмотров: 5
Описание:
Na Cales Katemana
Katika jamii nyingi za vijijini hapa Tanzania, mnyama punda ni nguzo muhimu ya maendeleo — akitumika kusafirisha maji, kuni, mazao ya shambani, na hata wagonjwa kwa umbali mrefu. Hata hivyo, kwa muda mrefu punda wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kuumizwa na kuharibiwa ngozi kutokana na matumizi ya zana duni au zisizofaa katika kubebea mizigo.
Ni katika muktadha huu, Shirika la INADES Formation Tanzania, kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya mifugo, limezindua kampeni maalum ya matumizi ya matandiko salama na rafiki kwa punda. Uzinduzi huu umefanyika katika kijiji cha Kinyamwenda, Wilaya ya Singida, ambapo punda wengi wamekuwa wakihusika moja kwa moja katika shughuli za kiuchumi za kaya.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: