RASTAFARI WATOA WITO WA AMANI NA UMOJA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025
Автор: CALES TV
Загружено: 2025-07-26
Просмотров: 76
Описание:
Jumuiya ya Rastafari kutoka maeneo mbalimbali nchini imekutanika katika kata ya Mpunguzi – Sabasaba, Dodoma kuadhimisha kumbukizi ya miaka 135 ya kuzaliwa kwa Mfalme Haile Selassie, kiongozi wa kihistoria kutoka Ethiopia anayeheshimiwa na Rastafari duniani.
Sherehe hiyo iliambatana na sala, maombi, burudani za reggae na maonyesho ya sanaa, huku ujumbe mkubwa ukiwa ni amani, mshikamano na heshima kwa kila mmoja kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
"Rasta si uhuni – ni mfumo wa maisha wa kiroho, unaojenga upendo, haki na maadili," alisema Ras Geoge, mwakilishi wa vijana.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Ras Mlulu (Dodoma), Ras Mambo (Dar), na Ras Geoge walipongeza serikali kwa kutambua uwepo wa Rastafari kama sehemu ya jamii inayochangia maendeleo ya taifa.
Wito wao kwa Watanzania: Tuwe na uchaguzi wa amani na mshikamano, kila mmoja awe balozi wa utulivu.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: