AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA NYUMBA YAKE MTWARA| MAJIRANI WAGUNDUA KUPITIA HARUFU NA NZI
Автор: Faida Online TV
Загружено: 2025-12-26
Просмотров: 2246
Описание:
Katika hali isiyo ya kawaida, Mwili wa Mwanamke mmoja aitwae Sofia Ismaili Kasimu (40) Mkazi wa Mtaa wa Mbae Mashariki, Manispaa ya Mtwara mikindani, umekutwa ndani ya Nyumba yake ukiwa tayari umeanza kuharibika baada ya Mama huyo kutoonekana hadharani kuanzia siku ya Jumatano ya Desemba 24 2025 huku majirani wakidai kuwa wameugundua mwili huo baada ya kuhisi harufu na Inzi kutoka kwenye Nyumba hiyo.
Wakiongea na Faida Online TV (watu wa Field) Baadhi ya Mashuhuda wamesema kuwa Bi, Sofia alikuwa na Ugongwa wa kuanguka yaani Kifafa na alikuwa akiishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo bila msaidizi yeyote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Mbae mashariki Ndugu Hamisi Athumani amesema kweli wameukuta Mwili huo ndani ya Nyumba hiyo na kisha kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara ambao walifika eneo la tukio na kushuhudia hali hiyo.
Tutaendelea kufuatilia taarifa hii kwa Jeshi hilo la Polisi ili kujua chanzo cha kifo hicho.
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: