HIVI NDIVYO MNADA WA KWANZA WA UFUTA ULIVYOFANYIKA LINDI
Автор: Hello Media
Загружено: 2025-06-09
Просмотров: 2828
Описание:
Mkoa wa Lindi leo June 9, umefanya mnada wa kwanza wa msimu wa mauzo ya ufuta kwa mwaka 2025/26 ambapo tani 3,113 zimeuzwa kwa bei ya juu ya shilingi 2,710 na bei ya chini ikifikia shilingi 2,510.
Mnada huo umefanyika umefanyika katika kijiji cha Ruhokwe kata ya Mnolela Halmashauri ya Mtama kupitia chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao kinachohudumia wakulima wa wilaya za Kilwa, Manipsaa ya Lindi na halmashauri ya Mtama.
Mnada huo umehudhiriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na ushirika wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack pampoja na wakulima kutoka katika maeneo jirani ya kijiji hicho.
Wakizungumza mara baada ya kufanyika kwa mnada huo baadhi ya wananchi waliohudhuria mnada huo wamesema wameridhika na bei zilotajwa katika mnada huo licha ya kuwa toafuati na matarajio yao.
Aidha mkuu wa mkoa wa Lindi amewasisitiza wakulima kulinda ubora wa mazao yao ili uwasaidie kupata bei za kuridhisha katika minada ijayo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: