SHULE ALIYOTOKA MW/KITI WA HALMASHAURI (W) MASASI, WANAFUNZI WADHIHIRISHA KUWA NGANGARI | MDAHALO.
Автор: MUUNGWANA ONE TV
Загружено: 2026-03-05
Просмотров: 59
Описание:
MDAHALO: MWENA DAY SEC.SCHOOL WAPAMBA MOTO🔥
Mada: Je ni Haki kuwa na usawa Kati ya wanawake na wanaume?
Kuelekea kilele Cha maadhimisho Siku ya wanawake Dunia, Kata ya Ndanda | 08 March 2026.
Viongozi wa kata ya Ndanda, wameandaa utaratibu jumuishi Katika kuelekea Siku hiyo, huku wakiandaa kundi la akina mama kushirikiana Pamoja na kuandaa mpango kazi wenye muonekano chanya kwa jamii yetu ya Ndanda na kwingineko
Wakati kundi hili la akina mama wakielekea siku yao maalumu ya akina Mama, 08 March 2026, walipata kuwaalika viongozi wengine wa kiume kwa ajili ya kushirikiana kwa ukaribu, kuboresha Ili siku yao ilete tija kwa jamii.
Viongozi ambayo walialikwa, (Me) ni Diwani wa kata ya Ndanda ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Masasi kwa Sasa, Afisa Mifugo wa kata ya Ndanda na viongozi wengine kadhaa.
Aidha, jambo lilioneka kuwa ni ndogo lakini kadri muda ulivyokwenda kuna mambo mengi makubwa yalitokea na pongezwa viongozi wetu kwa kuanzisha program hii kuelekea Siku ya maadhimisho siku ya wanawake dunia 08 March 2026.
Kundi lenye viongozi shupavu " Super Mama" wakishirikiana na baadhi ya viongozi wakiume waliopewa mwaliko, walitembelea shule ya Secondari Mwena Day na Zahanati ya Kijiji Cha Tuungane.
Katika maeneo hayo, Kiongozi mwenye dhamana Halmashauri ya wilaya ya Masasi Mh Bashiru Fakihi Mboneche, aliongoza zoezi la upandaji miti kuzunguka eneo la shule ya Secondari Mwena Day, na kutembelea zahanati ya Kijiji Cha Tuungane kuwaona wagonjwa. " Ni jambo mzuri na la kupongeza"
Mwisho wanawake Hawa Shupavu, walirudi tena shuleni kwa ajili ya Kipindi ambacho kiliandaliwa na shule juu ya mdahalo, mada iliyosema "Je haki kuwa na usawa Kati ya wanawake na wanaume"?
Na mwisho kabisa Mh. Bashiru Fakihi Mboneche, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi aliongea na kuomba watu wote tufuate yale yote mazuri yenye kuleta tija kwenye jamii yetu ya Tanzania.
Update
Muungwana One tv
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: