ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

HATIMAYE GARI LIMEPATIKA | MITSUBISHI OUTLANDER | MAKAMBAKO-NJOMBE

Автор: MUUNGWANA ONE TV

Загружено: 2026-02-08

Просмотров: 259

Описание: TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limefanikiwa kulikamata gari lililoibiwa aina ya Mitsubishi Outlander pamoja na mtuhumiwa mmoja, ambaye alikutwa akiwa na bastola ya kutengeneza kienyeji, baada ya kufanya msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa hao.

Tukio hilo linahusiana na wizi wa gari uliotokea tarehe 16/12/2025 saa 06:00 usiku, katika Mtaa wa Uwanjani, Tarafa ya Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe. Gari hilo aina ya Mitsubishi Outlander lenye namba za usajili T.897 EAC, chasis namba CW5W0008014 na engine namba 4B12AA5184, lenye thamani ya Shilingi 20,000,000/=, ni mali ya Jovin Kafana (37), mfanyabiashara (Agent) mkazi wa Tazara, Mji wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Songwe.

Gari hilo liliibiwa baada ya kuvamiwa na majambazi waliomtishia mmiliki kwa kutumia bastola hiyo ya kutengeneza kienyeji, na baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilianza mara moja jitihada za kuwatafuta watuhumiwa hao.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe liliendelea na msako mkali, na tarehe 06/02/2026 saa 17:30 jioni, askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe walipata taarifa za kiintelijensia kuwa gari hilo lipo Makambako Mkoa wa Njombe. Walipofika Makambako, walimkamata mtuhumiwa aitwaye Bashiru Madembwe (35), fundi magari wa Mkazi wa Makambako Mkoa wa Njombe, ambaye aliwapeleka askari kuwaonesha gari hilo alipolificha katika Kitongoji cha Ipilimo Kijiji Cha Iyai, Kata Ya Ihowanza, Tarafa Ya Malangali, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa.

Vilevile, Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja (jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya upelelezi) aliyehusika katika tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha lililotokea tarehe 04 Februari, 2026 saa 04:00 asubuhi, katika eneo la Kisimani, Mtaa wa Unyamwanga, Kata ya Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe.

Katika tukio hilo, mtuhumiwa huyo na wenzake walimfyatulia risasi Yengo Mwapina, mkazi wa Sogea, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe, na kumsababishia jeraha katika kiuno upande wa kushoto, pamoja na kumnyang’anya fedha kiasi cha Shilingi Milioni Hamsini na Nne za Kitanzania (54,000,000/=) akiwa anatokea benki ya NBC Tunduma.

Watuhumiwa hao bado wanashikiliwa kwa ajili ya mahojiano ili kubaini mtandao wao na watu wengine wanaoshirikiana nao katika vitendo vya ujambazi na unyang’anyi kwa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, na baada ya kukamilika kwa mahojiano hayo, hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa onyo kali kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo vya ujambazi, unyang’anyi kwa kutumia silaha na uhalifu wa aina yoyote kuwa hakuna mahali pa kujificha, kwani lina mtandao mpana wa kiintelijensia na linaendelea kufanya operesheni kali, ambazo ni endelevu na zisizotabirika pia linawaonya wahalifu wote kuwa mkono wa sheria ni mrefu, na yeyote atakayejihusisha na vitendo hivyo atakamatwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, vilevile linaendelea kuwaomba wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwani usalama ni jukumu la kila mmoja wetu.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Songwe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe SACP AUGUSTINO SENGA.

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
HATIMAYE GARI LIMEPATIKA | MITSUBISHI OUTLANDER | MAKAMBAKO-NJOMBE

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

MIAKA 54 YA LUGUMI, MAMBO ANAYOJUTIA, AMJIBU MWAKINYO KUDHAMINI NGUMI

MIAKA 54 YA LUGUMI, MAMBO ANAYOJUTIA, AMJIBU MWAKINYO KUDHAMINI NGUMI

LENA

LENA

Maajabu! Bibi azuia gari na pikipiki zisiondoke Stendi Arusha, ushirikina watajwa

Maajabu! Bibi azuia gari na pikipiki zisiondoke Stendi Arusha, ushirikina watajwa

MKE WA TAJIRI ALIYEMILIKI DUKA KUBWA NA MASHINE YA KUSAGA KWA MASHARTI MAGUMU AFUNGUKA MAZITO

MKE WA TAJIRI ALIYEMILIKI DUKA KUBWA NA MASHINE YA KUSAGA KWA MASHARTI MAGUMU AFUNGUKA MAZITO

Utumwa wa Saudi: KTN yafichua masaibu ya Wakenya wanaodai kunyanyaswa Saudi Arabia

Utumwa wa Saudi: KTN yafichua masaibu ya Wakenya wanaodai kunyanyaswa Saudi Arabia

MUSUKUMA AONESHA AMBULANCE ZAIDI YA 10, ANUNUA KWA FEDHA ZAKE KUWAPA WANANCHI HUDUMA ZOTE KUGHARAMIA

MUSUKUMA AONESHA AMBULANCE ZAIDI YA 10, ANUNUA KWA FEDHA ZAKE KUWAPA WANANCHI HUDUMA ZOTE KUGHARAMIA

PART 1 : DUDUBAYA AMKATAA MTOTO WAKE,,MIMI SIO BABA YAKO // NITAKUPITIA KAMA UPEPO,KAA MBALI NA MIMI

PART 1 : DUDUBAYA AMKATAA MTOTO WAKE,,MIMI SIO BABA YAKO // NITAKUPITIA KAMA UPEPO,KAA MBALI NA MIMI

WALIOJERUHI NA KUPORA MIL 54 TUNDUMA WAKAMATWA.

WALIOJERUHI NA KUPORA MIL 54 TUNDUMA WAKAMATWA.

JINSI MTOTO WA GADDAFI SAIF AL-ISLAM ALIVYOZIKWA KISHUJAA LIBYA, MAELFU WAMLILIA

JINSI MTOTO WA GADDAFI SAIF AL-ISLAM ALIVYOZIKWA KISHUJAA LIBYA, MAELFU WAMLILIA

TAHARUKI YAIBUKA MWANAMKE AKIDAIWA KUUZA ENEO la MAKABURI - MWENYEWE AJIBU TUHUMA na NYARAKA KIBAO..

TAHARUKI YAIBUKA MWANAMKE AKIDAIWA KUUZA ENEO la MAKABURI - MWENYEWE AJIBU TUHUMA na NYARAKA KIBAO..

РАССТРЕЛ БАНДЫ ЧИКУНОВА. Самая страшная бойня в истории 1990-х

РАССТРЕЛ БАНДЫ ЧИКУНОВА. Самая страшная бойня в истории 1990-х

JOTI KWELI KASHINDIKANA AFANYA VITUKO MBELE YA RAIS BILA UOGA...

JOTI KWELI KASHINDIKANA AFANYA VITUKO MBELE YA RAIS BILA UOGA...

UTABIRI WA MVUA ZA MASIKA (MACHI - MEI 2026)

UTABIRI WA MVUA ZA MASIKA (MACHI - MEI 2026)

PART 2 : DUDUBAYA ATANGAZA VITA NA MTOTO WAKE // MIMI FALA WAKO // USICHEZE NA MIMI PUMBAVU ZAKO...

PART 2 : DUDUBAYA ATANGAZA VITA NA MTOTO WAKE // MIMI FALA WAKO // USICHEZE NA MIMI PUMBAVU ZAKO...

Przedwojenna Kronika lat 30 – Odcinek I

Przedwojenna Kronika lat 30 – Odcinek I

BALAA LA MAKOMANDO NA WALINZI WALIVYOMLINDA RAIS SAMIA AKIWASILI KARIAKOO USIPIME

BALAA LA MAKOMANDO NA WALINZI WALIVYOMLINDA RAIS SAMIA AKIWASILI KARIAKOO USIPIME

Merinding‼️Detik Detik Mengerikan Truk Patah As di Tanjakan Sitinjau Lauik, Lalu Lintas Lumpuh Total

Merinding‼️Detik Detik Mengerikan Truk Patah As di Tanjakan Sitinjau Lauik, Lalu Lintas Lumpuh Total

Ayatollah Ali Khamenei ni nani? Fahamu historia ya Kiongozi huyu Mkuu wa IRAN

Ayatollah Ali Khamenei ni nani? Fahamu historia ya Kiongozi huyu Mkuu wa IRAN

ГДЕ И КАК ЖИВУТ ПОЖИЛЫЕ В АВСТРАЛИИ

ГДЕ И КАК ЖИВУТ ПОЖИЛЫЕ В АВСТРАЛИИ

ASKARI POLISI WALIOMUA MFANYABISHARA WA MADINI WAHUKUMIWA KUNYONGWA MTWARA

ASKARI POLISI WALIOMUA MFANYABISHARA WA MADINI WAHUKUMIWA KUNYONGWA MTWARA

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]