MHE. MTAKA AWAPONGEZA WALIMU KWA KUIPELEKA NJOMBE KILELENI KIELIMU
Автор: CBK NEWS ONLINE
Загружено: 2025-07-12
Просмотров: 58
Описание:
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amewapongeza walimu na wadau wa elimu kwa mchango wao mkubwa uliosaidia kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika ngazi mbalimbali za elimu. Mhe. Mtaka alitoa pongezi hizo Julai 11, 2025, katika kikao cha tathmini ya matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kikiwakutanisha viongozi wa elimu kutoka ngazi ya shule, halmashauri na mkoa.
Katika hotuba yake, RC Mtaka alieleza kuwa Mkoa wa Njombe unaendelea kufanya vizuri kitaifa, ambapo ufaulu wa kumaliza elimu ya msingi umeongezeka kutoka asilimia 88.7 mwaka 2023 hadi asilimia 89.3 mwaka 2024. Kwa upande wa kidato cha nne, ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 93.5 hadi 94.3, na kwa kidato cha sita umefikia asilimia 99.9 mwaka 2025 kutoka 99.86 mwaka 2023.
Ameeleza kuwa kiwango cha ufaulu kwa wastani wa GPA kimeimarika, ambapo mwaka 2024 ilikuwa 2.6163 ikilinganishwa na 2.4796 mwaka 2025, ikiwa ni ongezeko chanya la 0.1368. “Mkoa wa Njombe unashindana na mikoa yoyote nchini kwa ubora wa elimu. Hili ni zao la juhudi zenu walimu, viongozi na wadau wote wa elimu,” alisema RC Mtaka kwa msisitizo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: