MHE. JOCTAN MTEWELE AWASILISHA MCHANGO WA MBUNGE MWANYIKA UJENZI WA KANISA KKKT MAGODA - NJOMBE
Автор: CBK NEWS ONLINE
Загружено: 2026-02-08
Просмотров: 19
Описание:
Diwani wa Kata ya Uwemba, Mhe. Jocktan Mtewele, Februari 08, 2026, amemwakilisha Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Mhe. Deo Mwanyika, katika Ibada ya Jumapili huku akisema Mchango huo ni sehemu ya ahadi ya Mhe. Deo Mwanyika kwaajili ya Umaliziaji ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Magoda.
Katika hafla hiyo, Mhe. Mtewele amekabidhi mchango wa Mbunge uliolenga kuendeleza ujenzi wa kanisa hilo, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mhe. Mwanyika wakati wa ziara zake za kikazi mwishoni mwa mwaka 2025.
Akizungumza kwa niaba ya Mbunge, Mhe. Mtewele ameeleza kuwa Mhe. Mwanyika anatambua umuhimu wa nyumba za ibada katika kujenga maadili na umoja wa kitaifa, hivyo ameguswa kuendelea kushirikiana na waumini hao mpaka kukamilika kwa nyumba hiyo ya Mungu.
Akitoa nukuu ya maneno ya Mbunge, Mhe. Mtewele alisema:
"Mheshimiwa Mbunge amenituma nifikishe salamu zake za upendo kwenu na amesema: 'Nilitamani kuwa nanyi leo, lakini majukumu yamenizuia. Hata hivyo, moyo wangu uko nanyi katika ujenzi huu. Ahadi niliyoitoa mwishoni mwa mwaka jana ni deni langu kwenu, na leo nawasilisha mchango huu kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zenu. Kanisa ni wadau wetu wakubwa katika maendeleo, na nitaendelea kushirikiana na waumini wa madhehebu yote bila ubaguzi katika kuijenga Njombe yetu.'"
Aidha, Mhe. Mtewele aliongeza kuwa Mbunge Mwanyika amekuwa akishirikiana kwa karibu na waumini wa dini zote katika jimbo la Njombe, akiamini kuwa maendeleo ya kijamii na kiroho yanategemeana. Alisisitiza kuwa ofisi ya Mbunge itaendelea kuwa wazi kusikiliza na kusaidia changamoto mbalimbali za wananchi katika sekta zote.
Kwa upande wao, waumini na uongozi wa Kanisa la KKKT Magoda wamemshukuru Mhe. Deo Mwanyika kwa kutimiza ahadi yake, wakisema kuwa mchango huo utakuwa chachu ya kuharakisha hatua za ujenzi zilizobaki.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: