MHE. HEMED AWATAKA WAFANYABIASHARA KUTOPANDISHA BEI ZA VYAKULA RAMADHANI
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-03-07
Просмотров: 78
Описание:
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewataka wafanyabiashara kutopandisha bei za bidhaa za vyakula ili kila mwananchi aweze kujikimu, hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Ametoa wito huo wakati akiwasalimia waumini katika Masjid SOGEA uliopo SOGEA Branch, Wilaya ya Mjini Unguja, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Swala ya Ijumaa.
Alhajj Hemed amesema mwezi wa Ramadhani ni kipindi muhimu cha kuchuma thawabu kwa kufanya mema, kusaidiana na kuhurumiana miongoni mwa jamii. Hivyo amewataka wafanyabiashara kufuata bei elekezi za bidhaa ili kuwapa wananchi nafuu ya kupata mahitaji yao ya iftari bila usumbufu.
Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya wafanyabiashara na wananchi katika kipindi hiki cha Ramadhani utasaidia kudumisha upendo, mshikamano na ustawi wa jamii.
#ASAMOnlineTV
#Ramadhani
#BeiZaVyakula
#Zanzibar
#UmojaNaMshikamano
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: