RASMI WIZARA YA ELIMU ZANZIBAR KUONDOA MFUMO WA "SHIFT" KWA WANAFUNZI
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-03-07
Просмотров: 1951
Описание:
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohammed Mussa amesema Serikali ya Awamu ya Nane inaendelea kuweka mkazo mkubwa katika ujenzi wa madarasa na skuli mpya ili kuimarisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Mhe. Lela ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika ukumbi wa Rahaleo Studio, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema juhudi hizo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuondoa mfumo wa zamu (shift) katika skuli pamoja na kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.
Aidha, amesema katika kutambua umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya taifa, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imeelekeza ujenzi wa jumla ya madarasa 1,000 kwa ngazi ya elimu ya msingi na madarasa 1,000 kwa elimu ya sekondari.
Vilevile, mpango huo unajumuisha ujenzi wa skuli 10 za ghorofa kwa kila ngazi ya elimu, hatua inayolenga kuongeza nafasi za wanafunzi na kuboresha zaidi sekta ya elimu nchini.
#ASAMOnlineTV
#ElimuZanzibar
#Siku100ZaUongozi
#MaendeleoYaElimu
#Zanzibar
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: