WAZIRI SHARIF AELEZA MAFANIKIO YA SEKTA YA VIWANDA BAADA YA SIKU 100 ZA UONGOZI
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-03-05
Просмотров: 32
Описание:
Mhe. Sharif Ali Sharif, Kaimu Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha siku 100 za uongozi wa Rais Hussein Ali Mwinyi, akibainisha hatua madhubuti zinazochukuliwa kuimarisha sekta ya viwanda nchini.
Akizungumza kuhusu maendeleo ya viwanda, Mhe. Sharif amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa Mradi wa Maeneo ya Viwanda Dunga Zuze, ambapo kwa sasa miradi mitatu ya viwanda inaendelea kutekelezwa kikamilifu.
Kwa upande wa Kisiwa cha Pemba, amefafanua kuwa Serikali inaendeleza mradi wa kimkakati wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata mwani katika eneo la Chamanangwe, Mkoa wa Kusini Pemba. Mradi huu unatarajiwa kuongeza thamani ya zao la mwani, kuinua kiuchumi wakulima wa mwani, na kufungua fursa mpya za masoko ya ndani na nje ya nchi.
#ASAMOnlineTV
#SektaYaViwanda
#Pemba
#DungaZuze
#MaendeleoZanzibar
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: