ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

MWENYEKITI CCM WILAYA YA HANDENI ANAVYOTUMIKA NA MBUNGE WA JIMBO LA HANDENI MJINI KUWATISHA

Автор: Gift Tv

Загружено: 2025-06-04

Просмотров: 477

Описание: MWENYEKITI CCM WILAYA YA HANDENI ANAVYOTUMIKA NA MBUNGE WA JIMBO LA HANDENI MJINI KUWATISHA WANACHAMA WA CCM HANDENI MJINI.
WAKATI siku za Wabunge kuendelea kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao Bungeni zikihesabika, joto limezidi kuwa kali kwa baadhi ya Wabunge hao baada ya kuwa na wasiwasi na hatima yao na uhakika wa kurejea Bungeni.

Hatua hii inapelekea baadhi ya Wabunge wasiokubalika katika majimbo yao kwa kutofanya kazi za kuridhisha nakuwa na mahusiano mabaya na wananchi katika miaka mitano tangu walipochaguliwa na sasa kuwatafuta viongozi wa chama kwa gharama kubwa wawabebeshe mzigo wa lawama ili kuona uwezekano wa kuwadanganya tena wananchi wawachaguwe na kurejea mjengoni.

Jimbo la Handeni mjini mkoani Tanga ni jimbo linaloongozwa na Mbunge Reuben Mtahamanilo Kwagilwa (CCM).

Mbunge huyo baada ya kuona hatima yake kuwa ndogo sasa ameanza kumtumia Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Handeni, Amiri Changogo na mwenezi wa wilaya, Mkobe kuwatisha wanachama wote wa chama hicho wenye nia ya kugombea jimbo hilo mwaka huu.

Viongozi hawa wameahidiwa zawadi nono endapo Kwagwilwa atarudi bungeni.

Akitoa taarifa kwa masikitiko makubwa, Mmoja wa rafiki wa karibu zaidi na Mbunge huyo ambae ni Diwani katika Halmashauri ya Mji Handeni, amesema ni kweli Mbunge amekuwa akimtumia Mwenyekiti wa CCM kuwatisha viongozi wa kata ,matawi na wajumbe kwa ujumla.

Alisema kuwa, Mwenyekiti ndio mwenye kauli ya mwisho yaani mtu wa mwisho kusema katika chama ambapo Wajumbe wamekuwa wakimshangaa sana Mwenyekiti wao huyo kuwa mtu tofauti na alivyokuwa awali.

Mmoja wa wanachama wa CCM kutoka kata ya Chanika alisikika akisema “Sisi wanachama wa CCM ambao tuna nia ya kugombea katika jimbo la Handeni mjini hatuna amani kabisa kwani Mwenyekiti wa CCM amekuwa akitumika na Mbunge vibaya kututisha endapo tutagombea na ameahidi kuwa atahakikisha tunafukuzwa ndani ya chama kabla ya muda wa uchaguzi ambapo hii ni kinyume na Katiba ya CCM inayomtaka kila mwachama anahaki ya kuchagua na kuchagulia” alisema mwana chama huyo.’’.

Mtoa taarifa ameendelea kudai kuwa, Mbunge amekuwa akimtumia Mwenyekiti huyo nyakati za usiku kuwafuata Wajumbe na kumwombea msamaha Mbunge huyo ambaye ameonyesha kutokuungwa mkono na watu wengi kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yake, kushindwa kutimiza ahadi zake pamoja na kujikweza baada ya kupewa nafasi hiyo.

Msemaji amesema pia alitumia nafasi hii kuwaomba Viongozi wa CCM ngazi ya Mkoa wa Tanga na Taifa kumuonya Mwenyekiti huyo kuacha kutumika kwa maslahi ya mtu mmoja na badala yake asimame katika nafasi yake na kuwaachia wanachama haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa.

“Yani huku kwetu Mwanaccm ukionekana humuungi mkono Mbunge ni kosa utatafutiwa kila aina ya fitina ili kuhakikisha kuwa unamuunga mkono Mh Mbunge au Mwenyekiti wa CCM wilaya akushughulikie hii sio haki kabisa.

Alipotafutwa Mwenyekiti huyo kwa njia ya simu alisema kuwa, chama kinautaratibu wa kuwasemea viongozi waliopo madarakani kwani wametumwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi.

Changogo alisema kuwa, viongozi wanapokuwa madarakani wao kama viongozi wa chama wanawajibu wa kuwasapoti na pale wanapomaliza muda wao na Binge kuvunjwa ndio inakuwa kikomo cha kutowasemea.

"Siwatishi wanachama wengine wa CCM wenye nia ya kuchukua fomu pindi muda utakapofika kwani kufanya hivyo ni kukiuwa chama na Handeni kelele ni nyingi na nimeendelea kuvumilia kelele hizo" Alisema Changogo.

Mwisho

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
MWENYEKITI CCM WILAYA YA HANDENI ANAVYOTUMIKA NA MBUNGE WA JIMBO LA HANDENI MJINI KUWATISHA

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

ZIARA YA KIKAZI MKOANI UFUNGUZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA HANDENI-MKATA

ZIARA YA KIKAZI MKOANI UFUNGUZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA HANDENI-MKATA

MKUU WA MKOA WA TANGA AIPONGEZA HANDENI DC KWA KUSIMAMIA MIRADI YA SERIKALI VIZURI .

MKUU WA MKOA WA TANGA AIPONGEZA HANDENI DC KWA KUSIMAMIA MIRADI YA SERIKALI VIZURI .

HALI ILIVYOKUWA ARUSHA BAADA YA MAKONDA KUTANGAZWA MSHINDI/WAJUMBE WASHINDWA KUJIZUIA

HALI ILIVYOKUWA ARUSHA BAADA YA MAKONDA KUTANGAZWA MSHINDI/WAJUMBE WASHINDWA KUJIZUIA

ENG KUNDO AELEZA SABABU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BARIADI MJINI .

ENG KUNDO AELEZA SABABU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BARIADI MJINI .

MACHO YOTE HAPA VIG0G0 WACHUKUA FOMU MAPEMA ACHA

MACHO YOTE HAPA VIG0G0 WACHUKUA FOMU MAPEMA ACHA

REUBEN KWAGILWA – Mbunge wa jimbo la Handeni mjini.

REUBEN KWAGILWA – Mbunge wa jimbo la Handeni mjini.

HAWA HAPA VIGOGO WALIOLIWA VICHWA KUGOMBEA UBUNGE CCM WATANGAZWA LIVE NA KATIBU MUENEZI CCM TAIFA...

HAWA HAPA VIGOGO WALIOLIWA VICHWA KUGOMBEA UBUNGE CCM WATANGAZWA LIVE NA KATIBU MUENEZI CCM TAIFA...

Փաստորեն. ո՞վ է ստում՝ Թաթոյա՞նը, թե՞ իշխանությունը

Փաստորեն. ո՞վ է ստում՝ Թաթոյա՞նը, թե՞ իշխանությունը

HUYU NYERERE AMESHINDIKANA... TAZAMA ALICHOKIFANYA MBELE YA MKE WA WAZIRI MKUU SUMBAWANGA

HUYU NYERERE AMESHINDIKANA... TAZAMA ALICHOKIFANYA MBELE YA MKE WA WAZIRI MKUU SUMBAWANGA

UMMY MWALIMU AINGIA kwa KISHINDO! APEWA NAFASI KUGOMBEA JIMBO la TANGA MJINI - MWANA-FA - AWESO WAMO

UMMY MWALIMU AINGIA kwa KISHINDO! APEWA NAFASI KUGOMBEA JIMBO la TANGA MJINI - MWANA-FA - AWESO WAMO

MBUNGE WA HANDENI VIJIJINI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KWENYE KITUO CHA AFYA CHA MKATA.

MBUNGE WA HANDENI VIJIJINI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KWENYE KITUO CHA AFYA CHA MKATA.

VITONGOJI 55 HANDENI MKOANI TANGA HAVINA HUDUMA YA UMEME

VITONGOJI 55 HANDENI MKOANI TANGA HAVINA HUDUMA YA UMEME

🔴 #TBC LIVE: WAZIRI MKUU AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA SUMBAWANGA MJINI

🔴 #TBC LIVE: WAZIRI MKUU AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA SUMBAWANGA MJINI

MATOKEO RASMI YA JIMBO LA KINONDONI/ TARIMBA/ TIMOTH WAIBUKA KIDEDEA/ WILAYA YA KINONDONI....

MATOKEO RASMI YA JIMBO LA KINONDONI/ TARIMBA/ TIMOTH WAIBUKA KIDEDEA/ WILAYA YA KINONDONI....

📌

📌"Nipo Imara Kuwatumikia Wananchi"Mbunge Wa Moshi Mjini.

DC Handeni ashinda uchaguzi, Changogo Mwenyekiti mpya CCM

DC Handeni ashinda uchaguzi, Changogo Mwenyekiti mpya CCM

BILIONI 4 ZANUFAISHA WANAWAKE MKOA WA KATAVI

BILIONI 4 ZANUFAISHA WANAWAKE MKOA WA KATAVI

MAKONGORO NYERERE: ALIYEPIGWA RISASI TANO ZA KICHWA NINAHAMU KUBWA YA KUMUONA.

MAKONGORO NYERERE: ALIYEPIGWA RISASI TANO ZA KICHWA NINAHAMU KUBWA YA KUMUONA.

Hi ndio hatua ya kwanza kwenye Ukaguzi wa gari kitaalamu

Hi ndio hatua ya kwanza kwenye Ukaguzi wa gari kitaalamu

MBUNGE AAHIDI KUOGA HADHARANI MRADI WA MAJI UKIKAMILIKA

MBUNGE AAHIDI KUOGA HADHARANI MRADI WA MAJI UKIKAMILIKA

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]