Elimu ya Usalama Barabarani Yawafikia Wanafunzi wa Skuli ya Glorious
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-03-04
Просмотров: 110
Описание:
Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani imefanya ziara maalum katika Skuli ya Glorious kwa lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza ajali na kuongeza uelewa kuhusu matumizi sahihi ya barabara.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo Hakim Daudi Mwita, amesema kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaoendesha vyombo vya moto bila kuwa na elimu ya kutosha kuhusu sheria na kanuni za barabarani.
Ameeleza kuwa hali hiyo ni hatari na inaweza kusababisha ajali ambazo zingeweza kuepukika iwapo wanafunzi watapatiwa elimu sahihi mapema kuhusu matumizi salama ya barabara.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Hamza Mbaruk, amewaomba wazazi kuacha kuwapatia watoto wao vyombo vya moto bila kuhakikisha wamepata mafunzo pamoja na vibali vinavyotakiwa kisheria.
Nao wanafunzi wa skuli hiyo wameeleza kufurahishwa na elimu waliyoipata, wakisema kuwa itawasaidia kujilinda dhidi ya ajali pamoja na kuacha kuendesha vyombo vya moto bila kuwa na leseni halali.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: