DKT. KHALID: WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI YAPIGA HATUA NDANI YA SIKU 100 ZA RAIS MWINYI
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-03-03
Просмотров: 687
Описание:
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed, ameeleza dhamira na mafanikio yaliyofikiwa na wizara hiyo katika kipindi cha siku mia moja za uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Dkt. Khalid ameyasema hayo katika mahojiano yaliyofanyika Studio za Rahaleo, Mkoa wa Mjini Magharibi, akizungumzia mikakati ya wizara na utekelezaji wa malengo ya siku 100 za Rais.
Amesema wizara imejipanga kuanzisha ujenzi wa Chuo cha Mabaharia, ambacho kitakuwa chachu ya kuimarisha sekta ya usafiri wa baharini na kupanua fursa za ajira kwa vijana wa Zanzibar. Ameongeza kuwa chuo hicho kitasaidia kuongeza ujuzi wa wataalamu wa masuala ya bahari na kuchangia kukuza uchumi wa nchi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: