"WAZAZI MSIWAFICHE WENYE MAHITAJI MAALUM"
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-28
Просмотров: 362
Описание:
Mbunge wa Viti Maalum Kundi la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar, Yumna Mmanga Omar, amewataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaficha na kuwatenga watoto wenye ulemavu, akisisitiza kuwa wana haki sawa na watoto wengine katika jamii.
Akizungumza wakati wa hafla ya kutoa sadaka ya futari kwa familia 200 za makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu katika Skuli ya Salim Turky, Mpendae, Mkoa wa Mjini Magharibi, Yumna amesema watoto wenye ulemavu wanastahili kupewa fursa za elimu, malezi bora na maendeleo kama ilivyo kwa watoto wengine.
Ameeleza kuwa mtoto mwenye ulemavu ni sawa na mtoto mwingine yeyote, na anaweza kuwa na vipaji na uwezo mkubwa zaidi endapo atapatiwa malezi bora, elimu stahiki na kuaminiwa na jamii inayomzunguka.
Kwa upande wao, wananchi waliopatiwa msaada huo wamesema wamepokea sadaka hiyo kwa mikono miwili, wakibainisha kuwa familia nyingi zenye watu wenye ulemavu zinaishi katika hali ngumu ya kiuchumi, hivyo msaada huo umekuja wakati muafaka.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: