SMZ KUJENGA UWANJA WA NDEGE WA KISASA - NUNGWI
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-10
Просмотров: 1327
Описание:
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Mhe. Badria Attai Masoud, amekutana na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo ndani ya Wizara hiyo.
Akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Tatu la Abiria, Uwanja wa Ndege, amesema mkutano huo ni sehemu ya jitihada za wizara kukutana na vyombo vya habari ili kueleza maendeleo yaliyopatikana pamoja na mikakati iliyopo.
Ameeleza kuwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeandaa mikakati madhubuti inayolenga kuboresha sekta ya ujenzi na uchukuzi, kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii Zanzibar.
#UjenziNaUchukuzi #MaendeleoZanzibar #VyomboVyaHabari #AsamOnlineTV
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: