TAARIFA YATOLEWA KUHUSU MADAI YA UZEMBE YALIOSABABISHA VIFO VYA WATOTO, HOSPITALI ZA WILAYA
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-12
Просмотров: 5152
Описание:
Msimamizi wa hospitali za wilaya kutoka Saifee Hospital, Happiness Mashimba, ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hatua zilizochukuliwa kufuatia matukio mawili tofauti yaliyotokea katika Hospitali ya Wilaya ya Chumbuni na Kitogani.
Matukio hayo yanahusiana na madai ya wagonjwa kutopata huduma stahiki kutoka kwa wahudumu wa hospitali hizo, hali iliyopelekea vifo vya watoto wawili katika siku tofauti.
Amesema uongozi umechukua hatua za awali ikiwemo kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli wa matukio hayo na kuhakikisha uwajibikaji unafanyika kwa mujibu wa taratibu na sheria, pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma ili matukio kama hayo yasijirudie.
#Afya #Uwajibikaji #HudumaZaAfya #Zanzibar #AsamOnlineTV
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: