UPEPO MKALI WAEZUA PAA LA NYUMBA - ZANZIBAR
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-14
Просмотров: 316
Описание:
Kufuatia tukio la kuanguka kwa paa la nyumba ya Bwana Mzee Ali Makame katika Shehia ya Magomeni Uwandras, Wilaya ya Mjini Unguja, Asam Online TV imefika eneo la tukio kwa lengo la kufahamu chanzo cha tukio hilo pamoja na athari zilizojitokeza.
Akizungumza na Asam Online TV, Sheha wa Shehia hiyo, Ndugu Abdallah Ashkina, amesema alipokea taarifa za tukio hilo katika ofisi za shehia mara baada ya wananchi kutoa taarifa, na kueleza hatua zilizochukuliwa mara moja kuhakikisha usalama wa familia hiyo na mali zilizokuwemo ndani ya nyumba.
Juhudi za Asam Online TV hazikuishia hapo tu. Timu yetu pia imezungumza na mke wa Mzee Ali, Bibi Salma Ramadhan Miraji, ambaye amesema tukio hilo limewashtua sana kwani limetokea ghafla bila dalili yoyote ya awali. Ameeleza kwa masikitiko jinsi tukio hilo lilivyotokea na changamoto walizokumbana nazo mara baada ya paa hilo kuanguka.
Taarifa zaidi juu ya chanzo halisi cha tukio hilo zinatarajiwa kutolewa baada ya uchunguzi wa kina kukamilika.
#AsamOnlineTV #HabariZaMtaa #MagomeniUwandras #MjiniUnguja
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: