UJENZI NA UUZWAJI VIWANJA FUONI KIBONDENI WASITISHWA BAADA YA MGOGORO
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-14
Просмотров: 1154
Описание:
Shughuli za ujenzi na uuzaji wa viwanja vya Bw. Ahmed vilivyopo Fuoni Kibondeni zimesimamishwa kwa muda kufuatia mvutano kati ya mmiliki wa eneo hilo na dalali wake, huku hatua za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa ili kumaliza mgogoro huo.
Taarifa zinaeleza kuwa sintofahamu hiyo imetokana na kutokuelewana katika makubaliano ya kimkataba, hali iliyoibua utata juu ya umiliki na uendelezaji wa eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mohamed Ali, alifika eneo la tukio na kufanya mazungumzo na pande zote mbili, ambapo walikubaliana kusitisha kwa muda shughuli zote hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi wa kisheria.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B”, Amour Mmanga, pamoja na Sheha wa Kibondeni, Iddi Abdallah Haji, walimpongeza Mkuu wa Mkoa kwa kuingilia kati, wakisisitiza umuhimu wa kulinda amani katika eneo hilo linalokua kwa kasi kwa makazi na uwekezaji.
Mmiliki wa shamba, Ahmed Salim Mbarouk, amesema chanzo cha mgogoro ni kutofautiana kwa makubaliano na dalali wake, huku dalali huyo akiahidi kukaa mezani ili kufikia muafaka wa kudumu.
#FuoniKibondeni #MigogoroYaArdhi #MjiniMagharibi #AsamOnlineTV
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: