Mkataba wa aina yake wa kimataifa wa kuhifadhi viumbe hai baharini kuanza kutekelezwa
Автор: Habari za UN
Загружено: 2026-01-15
Просмотров: 46
Описание:
#HabarizaUN #UmojawaMataifa #Kiswahili #UNNewsKiswahili
Baada ya takriban miongo miwili ya maandalizi,hatimaye Mkataba wa Kimataifa wa kulinda viumbe hai wa baharini kwenye Bahari Kuu, BBNJ unaanza kutumika tarehe 17 mwezi huu wa Januari. Hii ni baada ya mataifa 81 kati ya 140 yaliyotia saini mkataba huo, kuuridhia. Mkataba unawezesha usimamizi wa pamoja wa eneo la Bahari Kuu, ambako rasilimali zake ni pamoja na samaki na dutu za kijenetiki zinazotumika kwenye dawa, vitu ambavyo havipatikani kwenye eneo la baharí lililo kwenye mamlaka ya nchi moja moja. Sasa kuanza kutumika mkataba huo kuna maana gani? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Mzee Ali Haji, Naibu Katibu Mkuu anayehusika na Katiba na Sheria katika Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nchini Tanzania. Yeye aliongoza jopo la wataalamu wa Tanzania kwenye mjadala wa mkataba huu. Anaanza kwa kuelezea anapokea vipi hatua hii.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: