UJENZI WA JENGO LA HUDUMA ZA HARAKA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WAGONJWA
Автор: KUSINI NEWS
Загружено: 2026-02-05
Просмотров: 31
Описание:
UJENZI WA JENGO LA HUDUMA ZA HARAKA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WAGONJWA
Serikali imetoa shilingi milioni 41.1 kutekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la huduma za haraka (Fast truck) katika kituo cha Afya Mjimwema manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Kamati ya siasa Mkoani Ruvuma ikiongozwa na Mwenyekiti wake Komred Oddo Mwisho imetembelea na kukagua mradi huo ambao umeboresha kasi na ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wateja kwa kuwapokea,na kuwahudumia wateja hivyo kupunguza msongamano wa wagonjwa.
Kamati ya Siasa inakagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma. Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya CCM
Kituo cha afya Mjimwema ni miongoni mwa vituo 31 vya kutolea huduma vilivyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: