MAHAKAMA KUU ZANZIBAR YATUPILIA MBALI MAOMBI YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MAJIMBO NANE
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-03-06
Просмотров: 438
Описание:
Mahakama Kuu ya Zanzibar imetupilia mbali maombi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar yaliyohusu wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika majimbo nane ambayo ni Pangawe, Malindi, Makunduchi, Chumbuni, Mwanakwerekwe, Kiembe Samaki, Mkwajuni na Chaani.
Maombi hayo yalifunguliwa na baadhi ya waliokuwa wagombea wa nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama cha ACT-Wazalendo katika majimbo hayo ya Unguja, wakipinga matokeo ya uchaguzi baada ya kushindwa katika kinyang’anyiro hicho.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mhe. Moh’d Ali Moh’d, ambapo mahakama imeamua kufuta mashauri hayo baada ya kuyapitia na kuyafanyia tathmini kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.
Mahakama ilikubaliana na pingamizi zilizowasilishwa na upande wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, kwamba maombi hayo yalikuwa na kasoro nyingi za kisheria.
Aidha, mahakama ilibainisha kuwa hati za kiapo (affidavits) zilizowasilishwa pamoja na maombi hayo zilikuwa na kasoro za kisheria, hali iliyosababisha hati hizo kutotambuliwa wala kutumika kama sehemu ya ushahidi katika maombi yaliyowasilishwa mahakamani.
Kutokana na kasoro hizo za kisheria, Mahakama Kuu ya Zanzibar iliamua kuyatupilia mbali maombi hayo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: