SUZA WAONESHA UTAIFA WA MATENDO: SEIC WAFANYA USAFI NA KUGUSA MIOYO YA WATOTO YATIMA MAZIZINI
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-16
Просмотров: 135
Описание:
Klabu ya Mazingira ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SEIC) kupitia Kampasi ya Habari Kilimani ya imefanya zoezi la usafi katika Nyumba ya Kulelea Watoto Yatima iliyopo Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mwenyekiti wa Klabu ya Mazingira ya SUZA Kampasi ya Kilimani, Ndg. Omar Shukuru Haji, amesema klabu hiyo imeamua kufanya usafi pamoja na kukabidhi vifaa vya kujifunzia kwa watoto wanaolelewa katika nyumba hiyo kwa lengo la kurejesha faraja na kuwafanya watoto hao kujihisi kuwa ni sehemu ya jamii inayowajali na kuwathamini.
Ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kijamii ya wanafunzi wa SUZA, sambamba na kuhamasisha mshikamano, huruma, uwajibikaji wa kijamii na utunzaji wa mazingira.
Zoezi hilo limepokelewa kwa furaha na uongozi wa nyumba hiyo pamoja na watoto, huku likiwa ni mfano halisi wa jinsi taasisi za elimu ya juu zinavyoweza kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii.
#SUZA #SEIC #UwajibikajiWaKijamii #Mazingira #AsamOnlineTV
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: