ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

Salama Na WALTER CHILAMBO SE6 EP59 | HABA NA HABA PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Автор: YahStoneTown

Загружено: 2023-03-20

Просмотров: 18391

Описание: #SalamaNa #SendTip MPESA #5578460
Pengine jina la episode hii linaweza likakupa muangaza kidogo wa story fupi ya maisha ya mgeni wetu wa wiki hii kwenye kiti chetu chakavu na meza ya kigae ambaye leo hii tayari kashaona, tochi ya maisha kwake inamulika tu vizuri na mbele anapaona. Huyu ni Walter Chilambo ambaye miaka tuseme 14 iliyopita alikua hana uhakika wa chakula chake cha siku tu achana na sehemu gani atalala. Ruka ruka ya kule na huku na bahati ya kupendwa alonayo na ambayo inaendelea mpaka leo naamini inakuja kwasababu ya ukarimu wake na hii ndo silaha yake yenye makali ambayo inampeleka mbali mpaka leo hii
Kama mtoto wa kiume ambaye unatakiwa kwenda kujitafuta ki maisha Walter nae ilibidi afanye yale yale ambayo si watoto wa kiume tu ila wengi wetu tumefanya ya kutaka kwenda kutafuta chako, na yeye aliona basi bora afanye hivyo. Safari ya kuja town kutoka mkoani anatuhadithia kwa upana kwenye episode hii. Mtu ambaye alimpokea ni mwana tu ambaye alienda nae shule moja, stop ya kwanza? Keko Magurumbasi. Na si kwamba alikua hana Ndugu hapa Dar es Salaam yeye alijiamulia isiwe hivyo, ilikua ngumu kumshashiwi Mama yake ambaye alitaka kujua ramani nzima ya mwanae ambaye alikua anakuja mjini kwa mara ya kwanza. Baada ya kufanikiwa kushawishi Mama Walter, kijana alipewa nauli na ananiambia by the time anafika Dar alikua na shilingi ELFU MOJA TU kwenye mfuko wake, hapo ni Ubungo kwenye stendi ya mkoa

Imani yake kwa Mungu wake pia ni silaha ya pili ya Ndugu Walter Chilambo. Hii ndo ambayo kwa mujibu wake imemsaidia kumvusha na mengi, maisha huko Keko hayakua mazuri, sikutaka kutumia neno si kama alivyo yatarajia maana hata yeye hakua na matarajio yoyote kwasababu alikua hajui anakutana na mazingira gani wakati anaenda kwa mwanae huyu aliyesoma nae Sekondari ambaye walikua na majina ya Baba yanayofanana. Mwenzetu anaitwa Michael. Alikaa pale huku akiwa anajaribu kuji tafuta ila kila anachogusa kilikua cha moto. Ananihadithia jinsi alivyoanza kufanya kazi za kila siku ili angalau apate hela ya kula, kule kwa Mama alikua anajifanya kama kila kitu kinaenda vizuri kwahiyo hata vimzinga vidogo vidogo vilikua haviendi. Ulipofika wakati wa yeye na mwanae Michael kufunguana mashati maana alikua ashakaa saana na hana dira nzuri hapo sasa ndo kila kitu kilianzia.

Unadhani mmoja anaweza kuwa na bahati kiasi gani kwamba mtu ambaye aliombwa amhifadhi kwenye ghetto lake wakati yeye anatafuta ustaarabu mwengine kuwa ni Ndugu yake? Pengine hii hutokea kwa wenye BAHATI TU, pengine Walter ni mmoja ya watu hao maana baada ya kujulikana hilo ndo angalau kukawa na ahueni ya kuwa na uhakika wa sehemu ya kuegesha mbavu, hii ni moja ya sehemu ilonisisimua kwenye simulizi yake, imagine mtu anavyokua kapigika alafu kutoka ambako hakujulikani mtu ambaye ameombwa akuhifadhi kwa muda anatokea kuwa ni Ndugu yako, hii ni Mwenyezi Mungu pekee ndo ambaye anaweza KUTENDA na kama utakua ushawahi kuishi kama ndege ambaye hajui analala wapi basi wewe utaweza kuelewa zaidi hapa.

Walter Chilambo ni mshindi wa Bongo Star Search wa mwaka 2012 na baada ya kushinda alianza safari yake ya muziki rasmi. Safari yake haikua ya urahisi kama ambavyo naamini alitarajia au sote tulidhani. Kiwanda cha Bongo Flava ki usalama tunaweza kusema kina wenyewe na ukiwa mpya kabla hujajua fagio lipi ndo linafaa kusafishia wapi basi kazi utakua nayo. Kwa Bwana Chilambo ambaye alishinda taji na pesa hakukua na tofauti kabisa. Neema kwa upande wake ilianza kuonekana baada ya yeye kuamua kufanya mziki wa kumtukuza Mungu na baada ya hapo mengine ni story tu.

Kwahiyo NINI hasa kilimfanya afanye maamuzi hayo? Kwenye kipindi ambacho kila mmoja ameamua kuimba nyimbo za mambo ya kitandani na mambo ya ndani je yeye kwanini aliamua kubadilisha gea? Maana Kama sauti anayo na kuandika anajua sasa sababu ni nini? Na pia wasiwasi wangu uko kwenye baada ya ‘kutoboa’ huko aliko na kupata umaarufu na sifa tele hatorudi tena huku kwenye kuimba nyimbo za kuachwa na kupendwa na kutendwa? Ana uhakika kiasi gani? Ukichukulia kama kuyaona na kuyafanya basi ashafanya mengi?
Nataka nikuachie hapa kwa leo ili uweze kwenda kuskiliza na kuya enjoy maongezi haya na mwanangu huyu ambaye hajabadilika, bado mcheshi, mwenye heshima na anayejitambua. Natumai hadithi yake itaku inspire kwa vile ambavyo ningependa iwe.
Amina.

Love,
Salama.

Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible & Msam...  

Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
Salama Na WALTER CHILAMBO SE6 EP59 | HABA NA HABA PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

Salama Na MASOUD KIPANYA SE6 EP60 | HERI KUFA MACHO… PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na MASOUD KIPANYA SE6 EP60 | HERI KUFA MACHO… PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

DIRA YA DUNIA BBC SWAHILI LEO 03/03/2026 Jumanne #bbcswahili #bbcswahilileo #dwkiswahili #habarileo

DIRA YA DUNIA BBC SWAHILI LEO 03/03/2026 Jumanne #bbcswahili #bbcswahilileo #dwkiswahili #habarileo

Salama Na ALLYBEE SE6 EP72| KULE NI KULE... PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na ALLYBEE SE6 EP72| KULE NI KULE... PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

BALAA! KAULI YA MWIGULU KUTOPENDWA NA SHANGWE KWENYE MSIBA WA PENGO/MAYALA ATIA NENO ZITO......

BALAA! KAULI YA MWIGULU KUTOPENDWA NA SHANGWE KWENYE MSIBA WA PENGO/MAYALA ATIA NENO ZITO......

Salama Na Masoud Kipanya

Salama Na Masoud Kipanya

TAARIFA YA HABARI - AZAM TV - 03/03/2026

TAARIFA YA HABARI - AZAM TV - 03/03/2026

Nandy Asante Baba (Behind The scene Part 02)

Nandy Asante Baba (Behind The scene Part 02)

Salama Na ALLYBEE SE6 EP72| KULE NI KULE... PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na ALLYBEE SE6 EP72| KULE NI KULE... PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

DW Kiswahili Habari za Ulimwengu | 03.03.2026 | Jioni | Swahili Habari leo | Podcast

DW Kiswahili Habari za Ulimwengu | 03.03.2026 | Jioni | Swahili Habari leo | Podcast

UTACHEKA ALICHOKISEMA ALLY KAMWE MBELE YA WAANDISHI WA HABARI | YANGA SOCCER SCHOOL

UTACHEKA ALICHOKISEMA ALLY KAMWE MBELE YA WAANDISHI WA HABARI | YANGA SOCCER SCHOOL

KWANINI TUNACHINJA MWEZI WA NNE ? PART 1

KWANINI TUNACHINJA MWEZI WA NNE ? PART 1

ბოლო ცნობები ახლო აღმოსავლეთიდან | პირდაპირი ჩართვა ისრაელიდან

ბოლო ცნობები ახლო აღმოსავლეთიდან | პირდაპირი ჩართვა ისრაელიდან

🔴TAARIFA YA HABARI YA SAA MBILI USIKU... MACHI 03, 2026

🔴TAARIFA YA HABARI YA SAA MBILI USIKU... MACHI 03, 2026

🔴LIVE:  MACVOICE AVUNJA UKIMYA,ANAFUNGUKA YOTE KUHUSU HATMA YAKE,NEXT LEVEL?

🔴LIVE: MACVOICE AVUNJA UKIMYA,ANAFUNGUKA YOTE KUHUSU HATMA YAKE,NEXT LEVEL?

DW Kiswahili Habari za Ulimwengu | 02.03.2026 | Jioni | Swahili Habari leo | Podcast

DW Kiswahili Habari za Ulimwengu | 02.03.2026 | Jioni | Swahili Habari leo | Podcast

Salama Na WANA SE6 EP75|  PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na WANA SE6 EP75| PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

BBC SWAHILI HALI INAZIDI KUWA TETE MASHARIKI YA KATI

BBC SWAHILI HALI INAZIDI KUWA TETE MASHARIKI YA KATI

Salama Na MFAUME MFAUME SE6 EP74| TOE - TO - TOE PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na MFAUME MFAUME SE6 EP74| TOE - TO - TOE PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

DW Kiswahili Habari za Ulimwengu | 01. 03. 2.2026 | Mchana | Swahili Habari leo | Podcast

DW Kiswahili Habari za Ulimwengu | 01. 03. 2.2026 | Mchana | Swahili Habari leo | Podcast

Salama Na JERRY SILAA SE6 EP22 FULL SHOW|KUKIWA JUA ,KUKIWA MVUAPART |SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na JERRY SILAA SE6 EP22 FULL SHOW|KUKIWA JUA ,KUKIWA MVUAPART |SendTip MPESA LIPA NO 5578460

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]