ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

Kwanini Uzaliwe Mara ya Pili? | Mwal. Eliya Lsn 2, 160925

Автор: Mwalimu Eliya

Загружено: 2025-12-21

Просмотров: 77

Описание: Hili ni jambo muhimu sana kwa anayejiita ama kutaka kuwa Mkristo

Em soma mwenyewe kisa hiki
Yohana 3:1-8 "Nikodemo Amwendea Yesu Usiku"

3 Yesu akamjibu, “Ninakwambia hakika, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.”
5 Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu.
Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

Wakati Yesu akizungumza na Nikodemo, alisema, “Amin, Amin, nakuambia: mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”. Nikodemo akamwambia, “Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” Yesu akajibu, “Amin, Amin, nakuambia: Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, ‘Hamna budi kuzaliwa mara ya pili…’ (Yohana 3:3-7, TMP).

Msemo “kuzaliwa mara ya pili” unamaanisha “kuzaliwa toka Kiroho” Nikodemo alikuwa na uhitaji wa kweli. Alihitaji mabadiliko ya moyo wake... Mabadiliko ya kiroho. Kuzaliwa upya, yaani kuzaliwa mara ya pili, ni kitendo au hatua ya Kiungu ambapo uzima wa milele hupewa mtu yule aaminiye (2 Wakorintho 5:17; Tito 3:5; 1 Petro 1:3; 1 Yohana 2:29; 3:9; 4:7; 5:1-4, 18). Yohana 1:12, 13 yaonyesha kuwa ”kuzaliwa mara ya pili” pia ina maana “kufanyika watoto wa Mungu” pale tuwekapo imani yetu katika jina la Yesu Kristo.

Yohana 1:12-13
12 Bali wote waliompokea na kumwamini aliwapa haki ya kufanywa watoto wa Mungu. 13 Hawa hawakuwa watoto wa Mungu kwa kuzaliwa kwa njia ya asili, wala kwa mapenzi au mipango ya watu bali wamezaliwa na Mungu mwenyewe. [si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. SUV]

Sasa swali lafuata, “kwa nini mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili?” Mtume Paulo katika Waefeso 2:1 asema, “Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu” (KCV). Kwa Warumi, aliwaandikia katika Warumi 3:23 akisema..., ”kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (TMP). Wenye dhambi ni wafu “kiroho”, lakini pale wanapopokea uzima rohoni kwa kumwamini Kristo, hapo ndipo Biblia hulinganisha jambo hilo na kuzaliwa mara ya pili. Wale tu waliozaliwa mara ya pili ndio wenye msamaha wa dhambi na uhusiano na Mungu.

Kama bado hujawahi kumwamini Bwana Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako, je utakuwa na utayari wa kumsikiliza Roho mtakatifu wakati akizungumza na moyo wako? Unahitaji kuzaliwa mara ya pili.
Je, ungependa utubu na ufanyike kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo hivi leo? Kumbuka “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12-13, TMP).

Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako na uzaliwe mara ya pili, Omba nami sala hii fupi. Kumbuka ya kwamba, kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haliwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumweleza Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupa wokovu. “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Naweka imani yangu Kwako pekee ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha-zawadi ya uzima wa milele! Amina!”

➲Ikiwa unapenda mafundisho yetu na ungependa kupata taarifa mpya kila wakati, tafadhali jiandikishe na ubonyeze kengele🔔 (karibu na kitufe cha kujiunga) ili kupokea taarifa mpya!!!

TAFADHALI KUMBUKA:
Mafundisho ama maoni yoyote kati ya yatayotolewa na wafundishaji si lazima yawakilishe maoni ya chaneli hii “Injili nje ya Kuta za Kanisa – inkmidia2007 “ au mafundisho mingine yoyote ambayo yanaweza kuwa au kusudiwa. Injili nje ya Kuta za Kanisa haiwatetei wala kuunga mkono shughuli yoyote isiyo halali ama inayokiuka sheria za nchi kwa mtu yeyote au jumuiya.

ILANI YA HAKI MILIKI:
Tunamruhusu mtu yeyote kutafsiri maudhui ya mafundisho yetu na kushirikisha wengine video lakini video lazima ibaki ikiwa na chapa chini “Injili nje ya Kuta za Kanisa – inkmidia2007 “ (yenye nembo yetu na kiunganishi cha chaneli hii) wazungumzaji wote wanapaswa pia kutambuliwa katika maelezo,

ZINGATIO: Hatufungani wala Kuchangamana na Taasisi, Dini ama Dhehebu lolote, kwetu ni nguvu za Mungu katika Neno lake!

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
Kwanini Uzaliwe Mara ya Pili? | Mwal. Eliya Lsn 2, 160925

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

Kuzaliwa Mara ya Pili Maana yake ni nini? | Mwal. Eliya Lsn 3, 160925

Kuzaliwa Mara ya Pili Maana yake ni nini? | Mwal. Eliya Lsn 3, 160925

Hotuba Ya SAMIA Yazua Mtafaruku Mkubwa | Mkakati wa Kumng'oa Wakabiliwa na Changamoto

Hotuba Ya SAMIA Yazua Mtafaruku Mkubwa | Mkakati wa Kumng'oa Wakabiliwa na Changamoto

Mkesha kuukaribisha mwaka Mpya Chumba Cha Mlima Wa Mizeituni.

Mkesha kuukaribisha mwaka Mpya Chumba Cha Mlima Wa Mizeituni.

29 декабря 2025 г.

29 декабря 2025 г.

Mbinguni, Kuzimu na Jehanamu [Ni wapi?] | Mwal. Eliya Lsn 1, 170925

Mbinguni, Kuzimu na Jehanamu [Ni wapi?] | Mwal. Eliya Lsn 1, 170925

Je, Tunaweza kumjua Mungu? | Mwl Eliya Lsn 1, 2025

Je, Tunaweza kumjua Mungu? | Mwl Eliya Lsn 1, 2025

Молодежь уходит из церкви! Разрыв поколений || Александр Шевченко

Молодежь уходит из церкви! Разрыв поколений || Александр Шевченко

LIVE: KINACHOFANYA FAMILIA NYINGI ZITESEKE

LIVE: KINACHOFANYA FAMILIA NYINGI ZITESEKE "PASTOR MGOGO

Biblia Ifunzavyo | Mwl. Eliya Lsn 1, 080625

Biblia Ifunzavyo | Mwl. Eliya Lsn 1, 080625

USIIZIKE NDOTO YAKO    (DON'T BURY YOUR DREAM) REV. DR. ELIONA KIMARO

USIIZIKE NDOTO YAKO (DON'T BURY YOUR DREAM) REV. DR. ELIONA KIMARO

FAHAMU NGUVU YA MAOMBI USIKU WA MANANE.

FAHAMU NGUVU YA MAOMBI USIKU WA MANANE.

Kuzaliwa Mara ya Pili Inamaanisha nini? | Mwal. Eliya Lsn 1, 160925

Kuzaliwa Mara ya Pili Inamaanisha nini? | Mwal. Eliya Lsn 1, 160925

TENGENEZA URAFIKI NA WATU WENYE AKILI WATAKUJA KUKUSAIDIA BAADAE

TENGENEZA URAFIKI NA WATU WENYE AKILI WATAKUJA KUKUSAIDIA BAADAE "PASTOR MGOGO

VITA VIPO LAKINI USHINDI NI LAZIMA  SEMINA YA NENO LA MUNGU 2025  MCH ABIUD

VITA VIPO LAKINI USHINDI NI LAZIMA SEMINA YA NENO LA MUNGU 2025 MCH ABIUD

Imani [Misingi yake ya Kweli] Mwl Eliya Lsn 1, 150925

Imani [Misingi yake ya Kweli] Mwl Eliya Lsn 1, 150925

Wokovu  -  Sehemu Ya 2 || Mawimbi ya Uamsho na Matengenezo

Wokovu - Sehemu Ya 2 || Mawimbi ya Uamsho na Matengenezo

Maneno Mabaya Yanavyoweza Kuharibu Maisha Yako

Maneno Mabaya Yanavyoweza Kuharibu Maisha Yako

Кто такой Святой Дух | Иоанна 14-16 | Гари Хэмрик

Кто такой Святой Дух | Иоанна 14-16 | Гари Хэмрик

1. MAOMBI YA TOBA YANAYOREJESHA ULICHOPOTEZA  // MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE.

1. MAOMBI YA TOBA YANAYOREJESHA ULICHOPOTEZA // MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE.

Biblia [Ni chakula cha Mwamini] Mwl ELiya Lsn 2, 220925

Biblia [Ni chakula cha Mwamini] Mwl ELiya Lsn 2, 220925

© 2025 ycliper. Все права защищены.



  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности



Контакты для правообладателей: [email protected]