ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

UGONJWA WA SONONA: Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

sonona

depression

dalili za sonona

matibabu ya sonona

tiba maongezi

dawa za sonona

usaidizi wa akili

mawazo ya kujiua

Автор: WikiElimu

Загружено: 2026-03-05

Просмотров: 52

Описание: Katika video hii inazungumza kuhusu sababu, dalili, matibabu, namna ya kuzuia, matarajio baada ya matibabu ya UGONJWA WA SONONA, endelea angalia mpaka mwisho kujifunza

Sonona (Depression) ni hali ya kuhisi huzuni, kushuka moyo na kukosa furaha. Wengi wetu tunajihisi huzuni au kukosa furaha kwa wakati mmoja au mwingine kwa muda mfupi. Lakini kwa mgonjwa wa sonona, hisia hizi zinakuwepo muda wote na kwa muda mrefu.
Ugonjwa wa sonona ni tatizo la kihisia, mgonjwa anahisi huzuni mwingi na hasira. Mfadhaiko wa aina hii unavuruga kabisa mfumo wa maisha ya kila siku wa mgonjwa.
Je! Nini dalili za sonona?
• Unapokuwa na sonona:
o Unakuwa na hali ya msononeko au hasira wakati wote
o Unapoteza hamu ya kufanya shughuli au mambo aliyokuwa akiyafurahia.
o Hapati usingizi au analala sana
o Anashindwa kula chakula kabisa au anakula muda wote – hii inaweza kusababisha akapungua sana uzito au kuongezeka uzito
o Anajihisi Uchovu na kukosa nguvu – hawezi hata kutoka kitandani
o Mgonjwa anajihisi kutokuwa na thamani yoyote, anajichukia, na anajihisi mwenye hatia
o Hapendi kufanya jambo lolote na anaepuka kufanya shughuli za kawaida
o Anajihisi kukata tamaa na bila msaada
o Anapata mawazo ya kifo au kujiua mara kwa mara
o Kutokujiamini ni swala la kawaida kwa mgonjwa wa sonona. Anaweza pia kuwa na hasira za ghafla na anakosa raha hata anapofanya mambo yanayopasa kumfurahisha – hata kujamiiana hakumfurahishi.
o Watoto wenye sonona wanaweza wasiwe na dalili sawa na watu wazima. Angalia mabadiliko kwenye kazi za shule, usingizi, na tabia. Kama unashuku mwanao ana ugonjwa huu, ni muhimu kuongea na mtoa huduma wa afya.
Sonona husababishwa na?
• Baadhi ya watu wanarithi jeni zinazoongeza hatari ya kuwa na ugonjwa wa sonona. Tabia unazojifunza nyumbani pia zinaweza kuchangia watu wa familia fulani kuwa na sonona. Watu wanaozaliwa na jeni hizi wanaanza kuwa na ugonjwa huu baada ya tukio la kuhuzunisha linaloongeza msongo wa mawazo.
• Kutumia pombe kupita kiasi au kutumia madawa ya kulevya kunaweza kusababisha sonona
• Mgonjwa ya muda mrefu kama kansa, ukimwi, maumivu ya muda mrefu au magonjwa yanayosababisha ukose usingizi.
• Matukio magumu ya kimaisha pia yanaweza kusababisha ugonjwa wa sonona:
o Unyanyaswaji au kutelekezwa
o Kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi
o Kifo cha mke, mme, mtoo, jamaa au rafiki kipenzi
o Talaka, hii ni pamoja na talaka kwa mzazi
o Kufeli mitihani au kurudia darasa
o Kuugua kwa mwanafamilia
o Kupoteza kazi
o Kutengwa na jamii (hasa kwa wazee)
Wakati gani utafute matibabu ya haraka?
• Ukihisi au ukiwa na mawazo ya kujiua, mwambie mtu uliyekaribu yako au nenda katika kituo cha afya kilicho karibu yako.
• Mwone daktari kama:
o Unasikia sauti ambazo hazipo au watu wengine hawazisikii
o Unalia lia kila mara bila sababu yoyote
o Sonona imeathiri uwezo wako wa kufanya kazi, kusoma shule, au kuishi vyema na familia kwa zaidi ya wiki 2
o Kama unadhani moja ya dawa unazotumia zinakusababishia dallili za sonona. USIBADILI au USIACHE kutumia dawa yoyote bila kuzungumza na daktari
o Unafikiri unapaswa kupunguza kunywa pombe, mwanafamilia au rafiki amekuomba kupunguza unywaji wa pombe, unahisi hatia kuhusu kiasi cha pombe unachokunywa, au unakunywa pombe asubuhi sana
Utambuzi
• Daktari ataongea na wewe kuhusu historia yako ya kiafya na familia yako, atakufanyia uchunguzi wa mwini na kuagiza vipimo kadhaa kama ikihitajika
• Daktari atagundua ukali wa ugonjwa wako (sonona inaweza kuwa kadri, wastani, au kali) na kisha atakueleza mpango wa matibabu.
Uchaguzi wa matibabu
Watu wengi wanaoishi na ugonjwa wa sonona, wanasema – ugonjwa wa sonona ni zimwi unalopambana nalo kila siku unapoamka mpaka unapoenda kulala – ni zito – na unahitaji msaada kulibeba.
Matibabu ya sonona yanategemea dalili ulizonazo – kama dalili ni za kadri– daktari anaweza kukupatia ushauri na kukufunza namna ya kujitunza mwenyewe ukiwa nyumbani – tutayazungumza mambo haya muda mfupi ujao.
Lakini kwa watu wenye Sonona ya wastani au kali – wanapatiwa dawa za kudhibiti sonona na tiba maongezi ''talk therapy''. Daktari anaweza kuamua kukupeleka kwa daktari bingwa wa magonjwa ya akili kama sonona yako ni wastani au kali, au kama matibabu anayokupatia hayasaidii.


Emmanuel Mniko #mniko #wikielimu @wikielimu

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
UGONJWA WA SONONA: Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

UGONJWA WA KISONONO: Sababu, Dalili, Matibu, Kuzuia

UGONJWA WA KISONONO: Sababu, Dalili, Matibu, Kuzuia

VVU/UKIMWI: Sababu, Dadilili, Matibu, Kuzuia

VVU/UKIMWI: Sababu, Dadilili, Matibu, Kuzuia

#LIVE: Misa Takatifu ya Jioni na Mafundisho ya Biblia Takatifu | Kanisa Kuu la Mt. Yosefu,  DSM.

#LIVE: Misa Takatifu ya Jioni na Mafundisho ya Biblia Takatifu | Kanisa Kuu la Mt. Yosefu, DSM.

Maria Sakkari vs. Iga Swiatek | 2026 Indian Wells Round 3 | WTA Match Highlights

Maria Sakkari vs. Iga Swiatek | 2026 Indian Wells Round 3 | WTA Match Highlights

Вертикальные Борозды на Ногтях – Что Они Значат и Когда Это Опасно

Вертикальные Борозды на Ногтях – Что Они Значат и Когда Это Опасно

KIUNGULIA: Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

KIUNGULIA: Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

MWALUNENGE ATUNISHA MFUKO WA MZRH WOMEN GROUP

MWALUNENGE ATUNISHA MFUKO WA MZRH WOMEN GROUP

MTINDIO WA UBONGO: Sababu, Dalili, Matibabu

MTINDIO WA UBONGO: Sababu, Dalili, Matibabu

Król Szwecji Karol XVI Gustaw z Prezydentem RP Karolem Nawrockim

Król Szwecji Karol XVI Gustaw z Prezydentem RP Karolem Nawrockim

Лечение грибка ногтей | Опасные ошибки, которые делают все

Лечение грибка ногтей | Опасные ошибки, которые делают все

🔴HAPA NA PALE KUTOKA SIMIYU, MACHI 10, 2026 -

🔴HAPA NA PALE KUTOKA SIMIYU, MACHI 10, 2026 -

MDOMO SUNGURA (Mdomo wazi): Sababu, Dalili, Matibabu

MDOMO SUNGURA (Mdomo wazi): Sababu, Dalili, Matibabu

Koronka do Bożego Miłosierdzia Teobańkologia 10.03 Wtorek

Koronka do Bożego Miłosierdzia Teobańkologia 10.03 Wtorek

MTOTO NJITI (Amewahi kuzaliwa): Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

MTOTO NJITI (Amewahi kuzaliwa): Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

MATANGAZO YA JIONI | 10 03 2026

MATANGAZO YA JIONI | 10 03 2026

MAFUA YA NGURUWE: Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

MAFUA YA NGURUWE: Sababu, Dalili, Matibabu, Kuzuia

DEGEDEGE: Sababu, huduma ya Kwanza

DEGEDEGE: Sababu, huduma ya Kwanza

Koniec z okularami? To jedno nasionko odbudowuje siatkówkę od wewnątrz

Koniec z okularami? To jedno nasionko odbudowuje siatkówkę od wewnątrz

KUONGEZEWA DAMU: Sababu, Matayarisho, Athari

KUONGEZEWA DAMU: Sababu, Matayarisho, Athari

MAUMIVU WAKATI WA HEDHI: Sababu , Dalili, Matibabu

MAUMIVU WAKATI WA HEDHI: Sababu , Dalili, Matibabu

© 2025 ycliper. Все права защищены.



  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности



Контакты для правообладателей: [email protected]