MWALUNENGE ATUNISHA MFUKO WA MZRH WOMEN GROUP
Автор: Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya
Загружено: 2026-03-07
Просмотров: 15
Описание:
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge, Ndg. Patrick Mwalunenge, amepongeza juhudi za Jumuiya ya Wanawake wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya (MZRH) kwa kutoa zawadi ya mashine ya kisasa ya kupima umeme wa kichwa (EEG) yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 67 kwa hospitali, ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya.
Ndg. Mwalunenge Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika hospitalini hapo, amepongeza hatua hiyo akisema inaonyesha uzalendo wa hali ya juu na utayari wa kuunga mkono maendeleo.
Katika kuunga mkono jitihada zao, Mwalunenge amechangia kiasi cha shilingi milioni 3 taslimu ili kuendeleza maendeleo ya umoja huo na kuahidi kuendelea kuwapa ushirikiano wa hali na mali.
Mashine hiyo ya EEG inatarajiwa kuboresha huduma za utambuzi wa magonjwa ya mfumo wa fahamu kwa wakazi wa kanda ya nyanda za juu kusini.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: