JAMAA AMRUSHIA NENO OMO - TUTAFUTIENI NCHI TWENDE
Автор: ZANZIBAR YETU
Загружено: 2025-09-28
Просмотров: 26562
Описание:
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, Jumapili ya leo (Septemba 28, 2025), ameitembelea bandari ya uvuvi na sehemu ya kuanikia dagaa ya Mchangani Pwani na Mangapwani Maotwe, katika shehia ya Mangapwani, Kaskazini B Unguja, kwa lengo la kujionea mwenendo wa shughuli na kuzungumza na wavuvi na wajasiriamali wa eneo hilo.
Ziara hiyo ambayo imejumuisha pia kusikiliza changamoto zao, ni muendelezo wake wa kukutana na makundi mbalimbali kwa lengo la kubadilishana mawazo na kuomba ridhaa yao ya kuwa Rais wa Zanzibar kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Wakizungumzia changamoto wanazokutana nazo hapo, Bw. Ramadhan Hassan Ramadhan, Bw. Salim Ali Khalfan na Bi Sauda Suleiman, wamesema wanakabiliwa na changamoto za mikopo yenye masharti makubwa, ambayo inawapa ugumu katika kufanikisha shughuli zao.
"Mheshimiwa hii ndio sehemu yetu ya kujipatia rizki, hapa kuna familia nyingi zinazotegemea eneo hili, lakini tumeshapewa taarifa ya kutaka kuhamishwa tukiambiwa eneo linataka kufanyiwa shughuli nyengine, na ukweli hatujui khatma ya maisha yetu". Wameelezea wajasiriamali hao.
Changamoto nyengine ambazo wameziwasilisha wavuvi na wajasiriamali hao mbele ya Mgombea, ni pamoja na kusumbuliwa na mamlaka za bahari wanapoingia Tanzania Bara, wakiambiwa leseni zao za uvuvi haziwezi kufanya kazi huko; uchache wa miundombinu ya vyoo na ukosefu wa maji safi na salama katika eneo hilo, ambalo ni jambo la muhimu ili kujiepusha na maradhi ya miripuko.
Nyengine ni kutokuwapata na kusikilizwa na viongozi wa nchi, hasa wanapowahitaji kuwaeleza changamoto zao; pamoja na kuchukuliwa ardhi zao za kilimo na kutumika kwa shughuli nyengine bila taratibu nzuri kupita.
Kwa upande wake, Mgombea huyo amesema Dhamira yake ni kulitumia vyema soko la mazao ya baharini ikiwemo dagaa kuwa soko kubwa Zanzibar.
Mgombea huyo amesema hio ni Fursa kubwa ya kiuchumi ambayo inahitaji uwezeshwaji wa Serikali ili kufikia matarajio.
Akieleza mipango yake ya uwezeshaji amesema "Kwanza tutaandaa mazingira bora ya uandaaji wa dagaa, tutatoa elimu juu ya kufanya bidhaa hii iwe bora na yenye kuwa na thamani ya kuingia katika soko la kimataifa, pamoja na uwezeshaji wa vifaa vya kisasa vya kufanikisha uandaaji mpaka kufika sokoni".
Aidha amesema Serikali yake itaifanya hio kuwa sekta rasmi ya kiuchumi na sio kimbilio la waliokosa ajira. "Tutawawezesha wajasiriamali hawa pamoja na kuandaa Hadhi ya dagaa la Zanzibar".
Othman ameitumia fursa hio kuomba ridhaa ya wananchi akisema hayo yote yatawezekana akiongoza Nchi hii.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: