MKURUGENZI AWAPONGEZA WATUMISHI IDARA YA AFYA, ATOA WITO KWA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI
Автор: Hanangdc Online Tv
Загружено: 2025-11-22
Просмотров: 88
Описание:
MKURUGENZI AWAPONGEZA WATUMISHI IDARA YA AFYA, ATOA WITO KWA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', Teresia Irafay amewapongeza watumishi wa afya kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato.
Pongezi hizo amezitoa Novemba 21, 2025 katika kikao kazi na waganga wafawidhi, watendaji wa kata na vijiji pamoja na wakuu wa idara kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Ukusanyaji wa mapato katika vituo vya afya kwa robo ya kwanza mwezi Julai -Septemba idara ya afya imekusanya shilingi 207,856,600 sawa na asilimia 103.87 ya shilingi 200,100,00 iliyolengwa.
Katika hatua nyingine, Irafay, amemuagiza mkuu wa divisheni ya utawala na lasilimali watu, kuwachukulia hatua za kinidhamu watendaji wa kata na vijiji ambao mapato yao yapo chini ya asilimia 25.
Kwa upande wake, mkuu wa divisheni ya utawala na lasilimali watu wa halmashauri, Gerald Mwarekwa amewataka watumishi kuzingatia miongozo ya utumishi wa Umma kwa kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: