BARAZA LA MADIWANI HANANG' LATOA 'HEKO' KWA MKURUGENZI KUSIMAMIA VIZURI MIRADI
Автор: Hanangdc Online Tv
Загружено: 2026-02-14
Просмотров: 40
Описание:
BARAZA LA MADIWANI HANANG' LATOA 'HEKO' KWA MKURUGENZI KUSIMAMIA VIZURI MIRADI
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' jana Februari 13, 2026 lilifanya mkutano katika ukumbi wa Halmashauri kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili (Oktoba- Desemba) 2025/2026.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. George Bajuta, ziliwasilishwa taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo Baraza la Madiwani limepongeza juhudi zinazofanywa na Halmashauri kwa kusimamia na kutekeleza miradi kwa ufanisi katika kata mbalimbali.
Madiwani wameeleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi pamoja na maboresho yanayoonekana katika utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: