PROGRAMU KABAMBE YA 'WASH' YATUA HANANG', WANANCHI GIDAMULA WAANZA KUNUFAIKA
Автор: Hanangdc Online Tv
Загружено: 2025-08-03
Просмотров: 169
Описание:
PROGRAMU KABAMBE YA 'WASH' YATUA HANANG', WANANCHI GIDAMULA WAANZA KUNUFAIKA
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, kwa kushirikiana na shirika la WaterAid na taasisi ya Prism Communication, inatarajia kutekeleza programu ya maji safi na usafi wa mazingira katika kata zote 33 za wilaya ya Hanang.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo katika kijiji cha Gidamula, kata ya Gidahababieg, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Teresia Irafay, amesema imani yake mradi huo utabadilisha tabia ya jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia usafi, kutumia vyoo bora na lishe inayozingatia makundi yote ya vyakula.
Aidha, amesema kuwa mradi utasaidia wananchi kupata huduma bora za maji na usafi ili kuimarisha afya za jamii.
"Mradi huu unatupa wakati mzuri wa kuwaelimisha wananchi hasa wanaoishi katika mazingira hatarishi ambayo yanatufanya tunapata magonjwa ambayo yanaepukika kama kipindupindu, magonjwa ya tumbo ambayo yanatokana na uchafu" amesema Irafay.
Akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi Pendo Mntambo kutoka Shirika la WaterAid amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha elimu ya usafi wa mazingira na kutoa mafunzo ya kubadili tabia kwa wananchi ili kulinda afya zao ambapo kwa kuanza wanajenga miundombinu ya choo katika shule ya Msingi Gidamula sambamba na huduma ya uvutaji wa maji.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: