BARIADI DC YAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 39.5
Автор: Bariadi DC
Загружено: 2026-02-06
Просмотров: 45
Описание:
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, leo Februari 06, 2026 limepitisha Mpango na Bajeti ya Mwaka 2026/2027 Jumla Tsh. 39,545,225,000 ambapo makadirio ya makusanyo ya mapato ya ndani Tsh. 3,164,032,000 ikiwa ni ongezeko la takribani shilingi Milioni 245.6 ya Bajeti ya makusanyo ya ndani ya mwaka 2025/2026.
Aidha katika Mwaka wa fedha 2026/2027 fedha inayotarajia kupokelewa kwaajili ya Miradi ya Maendeleo imekadiriwa kuwa Tsh. 9,453,263,000 na fedha ya Ruzuku ya Matumizi ya Kawaida imekadiriwa kuwa Tsh. 1,610,386,000.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mhe. Mayala Shiminji amesisitiza udhibiti wa vyanzo mbalimbali vya mapato ili makusanyo hayo yaweze kuhudumia mahitaji mbalimbali ya Halmashauri ikiwemo miradi ya maendeleo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: