MAMA AJIFUNGUA KICHANGA NA KUKIFUKIA PORINI MTWARA| CHAFUKULIWA NA MBWA WANANCHI WASHUHUDIA
Автор: Faida Online TV
Загружено: 2025-10-16
Просмотров: 3112
Описание:
Katika hali isiyo ya kawaida, Kichanga cha kiume kinachokadiriwa kuwa kimezaliwa Usiku wa jana Oktoba 15, 2025, kimekutwa pembezoni mwa Barabara kuu itokayo Mtwara kwenda Newala, Katika Kijiji cha Namahyataka Barabarani Kata ya Nanguruwe Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, huku kikiwa kimefukuliwa na Mbwa kutoka kwenye Shimo kilimofukiwa na Mama yake Mzazi huku ikiwa haijulikani kama kilifukiwa kikiwa hai au laa.
Faida Online TV ( Watu wa Field) Tumefika kwenye eneo hilo ili kujua undani wa tukio hilo, ambapo Wananchi mbalimbali wamezungumza kwa huzuni huku wengi wao wakijiuliza kwa nini amechukua uamuzi huo.
Nae Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara SACP Issa J. Suleimani, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiongeza kuwa tayari Mtuhumiwa ametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara.
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: