RC MRINDOKO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA MATENGENEZO YA BARABARA YENYE THAMANI YA BILIONI 1.6
Автор: KATAVI RS
Загружено: 2025-11-10
Просмотров: 229
Описание:
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, leo Novemba 10, 2025 ameshuhudia hafla ya utiaji saini wa mikataba ya matengenezo ya barabara inayotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika mkoa wa Katavi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, RC Mrindoko amesema mikataba hiyo ina thamani ya jumla ya shilingi bilioni 1.644, ambapo kati ya mikataba 10 iliyosainiwa, miradi sita yenye thamani ya shilingi milioni 171.08 imetolewa kwa vikundi maalum vya wanawake, vijana na wazee.
RC Mrindoko ameipongeza TARURA kwa hatua ya kuwashirikisha makundi hayo maalum katika miradi ya maendeleo, akisema hatua hiyo ni muhimu katika kuwawezesha kiuchumi na kuongeza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa miradi ya serikali.
“Mikataba hii inalenga kuboresha hali ya barabara zetu hasa katika msimu wa mvua, ili kuhakikisha usalama na kurahisisha shughuli za usafiri na uchumi katika Mkoa wa Katavi,” amesema RC Mrindoko.
Aidha, ametoa wito kwa TARURA kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa ubora, uwazi na thamani ya fedha, huku akiwataka wakandarasi kutotekeleza miradi kwa mazoea bali kwa weledi na uadilifu.
Vilevile, RC Mrindoko amewataka wakandarasi hao kutoa ajira kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi, hasa vijana, ili kuongeza kipato na kuchochea maendeleo ya jamii. Amesisitiza pia, Wakuu wa Wilaya washirikiane na TARURA katika kuwatambua, kuwawezesha na kuwajengea uwezo vijana na wanawake ili waweze kushiriki katika miradi midogo ya ujenzi kupitia vikundi vilivyosajiliwa kisheria.
Kwa upande wake, Meneja wa TARURA Mkoa wa Katavi, Mhandisi Innocent Mlay, amesema mikataba hiyo inatekelezwa katika halmashauri za Tanganyika, Mpanda Manispaa, Nsimbo, Mpimbwe na Mlele, na inafadhiliwa kupitia Mfuko wa Matengenezo ya Barabara (Road Fund).
Mhandisi Mlay ameongeza kuwa TARURA itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha barabara zinapitika muda wote na zinachangia katika kuimarisha shughuli za kiuchumi mkoani Katavi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: