E HABARI MARCH 10 2026/JUKWAA LA WATUMIAJI TANZANIA LASISITIZA WALAJI WAELIMISHWE HAKI ZAO
Автор: EFM TANZANIA
Загружено: 2026-03-10
Просмотров: 7
Описание:
JUKWAA la Watumiaji Tanzania (TCF) limesema bado kuna umuhimu wa kuongeza elimu kwa wananchi kuhusu haki zao kama walaji ili kujenga mazingira salama ya matumizi ya bidhaa na huduma nchini.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa TCF, Daudi Daudi, wakati akielezea kihusu maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Haki za Mtumiaji Duniani kwa mwaka 2026 yatakayofanyika Machi 15 jijini Tanga.
Daudi amesema maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo "Bidhaa Salama, Watumiaji Wenye Kujiamini" (Safe Products, Confident Consumers) ambayo inalenga kuhimiza upatikanaji wa bidhaa na huduma salama zinazozingatia viwango vya ubora ili kuwawezesha watumiaji kufanya maamuzi sahihi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: