MHE GONDWE AUNGANA NA RASI SAMIA KATIKA 27 YA KIJANI SINGIDA
Автор: Singidamc TV
Загружено: 2026-01-26
Просмотров: 53
Описание:
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe, ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika maadhimisho ya Siku ya 27 ya Kijani kwa kushiriki zoezi la upandaji miti pamoja na wananchi wa wilaya hiyo, ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Rais Samia.
Katika kuonesha mshikamano huo, Mhe. Gondwe ameongoza zoezi la upandaji wa miti 600 lililofanyika katika Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida, leo Januari 27, 2026, zoezi lililolenga kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kuimarisha uoto wa asili katika eneo hilo.
Zoezi hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia, pamoja na wadau wa mazingira, watumishi wa umma na wananchi, waliojitokeza kwa wingi kushiriki shughuli hiyo muhimu ya kimazingira.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Gondwe amesema Siku ya 27 ya Kijani imekuwa chachu ya kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira, akisisitiza kuwa upandaji miti ni nguzo muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Ameongeza kuwa Rais Samia ameendelea kuwa kinara wa uhifadhi wa mazingira kupitia kampeni ya 27 ya Kijani, inayotekelezwa kila mwezi nchi nzima kwa lengo la kuongeza uoto wa asili, kulinda rasilimali za mazingira na kuhakikisha kizazi cha sasa na kijacho kinaishi katika mazingira salama na endelevu.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: