MANISPAA YA SINGIDA YAZIDISHA MIKAKATI YA USAFI WA MAZINGIRA
Автор: Singidamc TV
Загружено: 2026-01-20
Просмотров: 56
Описание:
Manispaa ya Singida imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mji unaendelea kuwa safi kwa kuimarisha usimamizi wa taka na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira, amesema Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka, Makolo Shija. Alisema mikakati hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika kuhifadhi mazingira safi kwa kufuata taratibu sahihi za uhifadhi wa taka majumbani na katika maeneo ya biashara.
Alifafanua kuwa manispaa inaendelea kusimamia shughuli za usafi kila siku, hususan katika maeneo yenye shughuli nyingi za kibiashara kama masoko na stendi, huku akiwahimiza wananchi kuzingatia ratiba ya ukusanyaji wa taka katika mitaa yao ili kurahisisha zoezi hilo na kuzuia uchafuzi wa mazingira, akisisitiza kuwa ushirikiano wa jamii ni nguzo muhimu katika kulinda afya na usalama wa mazingira ya mji.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: