TARANGIRE KUPATA LANGO JIPYA LA MAMIRE
Автор: TANAPA DIGITAL
Загружено: 2026-03-13
Просмотров: 31
Описание: Kwa kuwa Hifadhi ya Taifa Tarangire ni ya pili kwa kuingiza watalii wengi zaidi kati ya Hifadhi za Taifa 21 zinazosimamiwa na TANAPA baada ya Hifadhi ya Taifa Serengeti, na ya tatu kwa wingi wa mapato yatokanayo na utalii baada ya Hifadhi za Taifa Serengeti na Kilimanjaro, hivyo kukamilika kwa Lango la Mamire Aprili 14, 2026 kutaifanya hifadhi hiyo kuwa na jumla ya Malango manne (4) na Uwanja wa ndege wa Kuro ambao pia hutumia kama lango kwa watalii wanaoshukia hapo, na kufanya maeneo ya kukatia vibali (permits) kuwa matano (5). Hii ni hatua kubwa sana, hivyo Lango hilo jipya litaongeza ufanisi, kupunguza idadi ya watalii katika malango mengine na kuwezesha utoaji wa huduma kwa haraka na kwa ubora zaidi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: