BREAKING: Pwani Kuzalisha Mboga na Matunda Kulisha Dar na Zanzibar – Waziri Chongolo Afunguka...
Автор: Habari Na Zaidi
Загружено: 2026-03-16
Просмотров: 2
Описание:
#HabariZaLeo #TanzaniaNews #KilimoTanzaniaKibaha,
Pwani – Machi 16, 2026
Serikali imeanza mkakati wa kuufanya Mkoa wa Pwani kuwa kitovu cha uzalishaji wa mboga mboga na matunda yatakayolisha masoko ya Dar es Salaam na Zanzibar. Hatua hiyo inalenga kuongeza uzalishaji wa mazao, kuimarisha usalama wa chakula na kufungua fursa zaidi za ajira kwa vijana na wakulima.
Akizungumza Machi 16, 2026 mjini Kibaha, Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo amesema Mkoa wa Pwani umechaguliwa kuwa mfano katika uzalishaji wa mboga mboga na matunda kwa kuzingatia ubora, viwango na tija ya kilimo.
Amesema mradi huo kwa awamu ya kwanza utaanza katika eneo la hekari 200 huku serikali ikiendelea kukamilisha taratibu na maandalizi ya utekelezaji wake.
Aidha, amesema mpango huo ni sehemu ya kutekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha uzalishaji wa chakula na kuhakikisha Tanzania inachangia kulisha Afrika na dunia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema mpango huo pia unalenga kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuongeza ajira kwa vijana kupitia sekta ya kilimo.
Ameeleza kuwa Wilaya ya Kibaha ina zaidi ya hekari 1,000 zinazofaa kwa kilimo hicho ambapo kwa kuanzia zitatumika hekari 200, huku Wilaya ya Kisarawe ikiwa na takribani hekari 1,500 zitakazotumika kwa kilimo cha umwagiliaji mwaka mzima kwa kuzingatia utaalamu wa kisasa wa kilimo.
Usisahau:
👍 Like
💬 Comment
🔔 Subscribe kupata habari na taarifa muhimu kila siku.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: