RAIS DKT. SAMIA AZINDUA SHULE 302 ZILIZOJENGWA NCHINI KUPITIA MIRADI YA BOOST NA SEQUIP
Автор: SINGIDA RS
Загружено: 2023-10-15
Просмотров: 506
Описание:
RAIS DKT. SAMIA AANZA RASMI ZIARA YA KIKAZI MKOANI SINGIDA
Miradi ya BOOST 2021/22 – 2025/26
Mkoa wa Singida ulipokea kiasi cha shilingi 9,024,600,000 kutoka Mradi wa BOOST kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya 12 za Msingi. Kati ya Shule hizo, shule 11 ni za mikondo miwili na shule 01 yenye mkondo moja. Kila Shule mpya yenye mikondo miwili ililetewa shilingi 493,400,000 ikiwa ni za ujenzi wa madarasa 16, Jengo la Utawala 01, matundu 24 ya Vyoo na Kichomea taka 01. Shule yenye Mkondo mmoja ililetewa shilingi 318,800,000 ikiwa ni za kujenga madarasa 09, matundu ya 16 ya vyoo, kichomea taka 01 na Jengo 01 la Utawala. Aidha, Shule 44 zimeongezewa miundombinu.
Baada ya kukamilika kwa Shule mpya 12 na Shule 44 zilizoongezewa miundombinu, wanafunzi 13,275 wa Elimu ya Awali na Msingi wamenufaika. Aidha, miundombinu hii imesaidia kupunguza msongamano katika baadhi ya Shule na wengine kupunguza umbali wa kutembea kwenda Shuleni.
MIRADI YA SERIKALI KUU YA UPANUZI WA SHULE ZA KIDATO CHA TANO NA SITA MWAKA 2023.
Mkoa wa Singida ulipokea kiasi cha shilingi 3,026,400,000 kutoka Serika Kuu kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu ya Shule za Sekondari za Kidato cha Tano na Sita Mwezi Mei, 2023. Miundombinu iliyojengwa ni mabweni 15, madarasa 44 na matundu 82 ya vyoo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: