🔴 BARAZA LA MADIWANI SONGEA MANISPAA LAPITISHA MAKADILIO YA BAJETI YA BILIONI 63
Автор: RUVUMA TV
Загружено: 2026-02-10
Просмотров: 64
Описание:
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma limeidhisha na kupitisha makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/27 yenye jumla ya shilingi bilioni 63.99.
Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 1.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26.
Kwa mujibu wa makadirio hayo, mapato ya ndani ya Manispaa yanatarajiwa kufikia shilingi bilioni 10. Aidha, shilingi bilioni 14 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, fedha ambazo zitapatikana kutoka vyanzo vya ndani, Serikali Kuu pamoja na wafadhili.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Bajeti, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea amewataka wataalamu wa Halmashauri kuwashirikisha madiwani kikamilifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.Meya huyo amesisitiza umuhimu wa uwazi na uwajibikaji, hasa katika utoaji wa taarifa za matumizi ya fedha za miradi, ili kuwawezesha madiwani kutekeleza vyema wajibu wao wa kuisimamia Serikali katika ngazi ya Halmashauri.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: