🔴 KUSILAWE ATAKA WANACHAMA CCM PERAMIHO KUUNGANA KUSAKA KURA ZA USHINDI
Автор: RUVUMA TV
Загружено: 2026-02-13
Просмотров: 29
Описание:
Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Alhaj Saad Sadiki Kusilawe, amewataka wanachama wa chama hicho katika Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma kushirikiana kwa umoja na mshikamano katika kuzisaka kura za ushindi kwa mgombea wa CCM kwenye uchaguzi mdogo unaofanyika jimboni humo tarehe 26 February
Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, marehemu Jenista Mhagama, ambaye alitokana na CCM.
Akizungumza katika mkutano na wanachama wa CCM Kata ya Mbinga Mhalule, Kusilawe amewataka wanachama kuvunja makundi na tofauti zozote zilizojitokeza wakati wa mchakato wa kura za maoni ndani ya chama, na badala yake kuwa mabalozi wa maendeleo yaliyotekelezwa na Serikali ya CCM ili kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo.
Amesema kuwa ushindi wa CCM utatokana na mshikamano, nidhamu na kujituma kwa kila mwanachama kuwafikia wananchi na kuwaeleza mafanikio ya Serikali katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Aidha, amewahamasisha wanachama pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi Februari 26 kupiga kura na kumchagua mgombea wa CCM, akieleza kuwa ushiriki wao ni muhimu katika kuendeleza gurudumu la maendeleo jimboni humo.
Kusilawe pia amesisitiza umuhimu wa kutunza amani na utulivu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi, akibainisha kuwa CCM ni chama kinavyotanguliza misingi ya amani, umoja na mshikamano kwa manufaa ya Taifa.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwaunganisha wanachama mara baada ya kumalizika kwa kura za maoni ndani ya chama, pamoja na kuwatia hamasa ya kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: