ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

VVU NA UNYONYESHAJI/WIKI YA UNYONYESHAJI IRINGA

Автор: Makutano TV

Загружено: 2021-08-08

Просмотров: 2617

Описание: Wiki hii ni wiki ya maadhimisho ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama Duniani maadhimisho ambayo kila Mwaka hufanyika kila mwaka tarehe 1-7 Julai.

Nchini Tanzania mkoa wa Iringa unaungana na wengine hapa Nchini kuadhimisha wiki hii ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama, lengo la siku hii ni kulinda , kuimarisha na kuendeleza unyonyeshaji wa maziwa ya mama.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga anasema Iringa inashika nafasi ya tatu kitaifa kwa tatizo la watoto wenye udumavu kwa asilimia 47.1 ikiongozwa na Mkoa wa Njombe sambamba na hilo anasema kuwa ni asilimia 66 ya watoto mkoani humo wananyonya maziwa ya mama pekee miezi 6 ya mwanzo.

Unyonyeshaji na VVU, Hatuwezi kuzungumzia wiki hii ya unyonyeshaji pasipo kulizungumzia kundi maalum la wakina mama wanaoishi na maambukizi ya VVU, je wao wanafanya nini katika kumlinda mtoto na kuhakikisha ananyonya miezi sita mfululizo?

Ni katika Mkoa wa Iringa mama ambaye hajataka jina lake kujulikana, mtoto wake ana umri wa chini ya miezi sita, anasema awali tangu kuzaliwa kwake hakuwahi kujua kama ameathirika mpaka alipougua sana ndipo mama yake akamfahamisha kwamba alizaliwa na maambuizi ya VVU, maisha yakaendelea kwa kuanza kutumia dawa, ” nilipata mchumba wa kwanza tulipoenda kupima alipojua nimeathirika akaniacha, anasema mama huyu, ndipo nilipata mwingine baadae na kuzaa naye mtoto, nilijifungua salama salmini na mtoto wangu ni mwenye afya kama mnavyo muona na sasa nasubiri kipimo kujua kama hakupata maambukizi au la…..”

Wahudumu wa afya ngazi ya jamii ndio wafuatiliaji wa afya kwenye kaya, Janerose Nyeho ni msimamizi wa wahudumu hao kutoka kituo cha Alamano

Lakini pia zipo changamoto

Zipo tofauti za unyonyeshaji kwa mtoto ambaye yuko kwenye hatari ya kuambukizwa, na mtoto ambaye amegundulika ana maambukizi, sambamba na hilo itokeapo mama ambaye ana maambukizi amepata michubuko kwenye matiti yake nini anapaswa kufanya bila kusahau lini mama huyu aache kunyonyesha? kutoka kituo cha afya cha Ngome Muuguzi kitengo cha afya ya mama na mtoto Yusta Materu anasema

Mwisho Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Elimu ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Esther Nkuba anasema serikali imeweka mikakati madhubuti kwa kutenga bajeti kwa watoa huduma ngazi ya jamii na huku akisisitiza wamama kuendelea kunyonyesha huku wakijikinga na UVIKO 19.

KAULI MBIU 2021 “KULINDA UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA NI JUKUMU LETU SOTE”

Kutoka Iringa Mimi ni Tukuswiga Mwaisumbe.

#wizarayaafyajiniawanawakenawatoto

#globalvolunteer

#rcpprogram

#taasisiyachakulanalishe

#lisheendelevu

#childrenincrossfare@watotowetutunuyetu

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
VVU NA UNYONYESHAJI/WIKI YA UNYONYESHAJI IRINGA

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

KADI YA ALAMA KUIMARISHA MFUMO WA TAARIFA ZA MTOTO IRINGA

KADI YA ALAMA KUIMARISHA MFUMO WA TAARIFA ZA MTOTO IRINGA

MRADI WA IEA - SOS  NA MANUFAA YA  KAMATI  ZA  MTAKUWWA

MRADI WA IEA - SOS NA MANUFAA YA KAMATI ZA MTAKUWWA

SERIKALI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MRADI WA WE CARE KWA  MALENGO  100%

SERIKALI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MRADI WA WE CARE KWA MALENGO 100%

JINSI YA KUPIKA  UJI WA MAPANDE KWA MTOTO

JINSI YA KUPIKA UJI WA MAPANDE KWA MTOTO

MFUMO WA M MAMA ULIVYO OKOA MAISHA YA MTOTO DERICK  - MUFINDI

MFUMO WA M MAMA ULIVYO OKOA MAISHA YA MTOTO DERICK - MUFINDI

KIPERA SHULE YA MSINGI  KONGWE NA MAPINDUZI YA ELIMU JUMUISHI

KIPERA SHULE YA MSINGI KONGWE NA MAPINDUZI YA ELIMU JUMUISHI

MIAKA 3 YA MRADI WA

MIAKA 3 YA MRADI WA "WE CARE " MKOMBOZI KWA WATOTO IRINGA

MATOKEO YA RIPOTI YA MFUMO WA NEVA / UFAHAMU/ WATOTO WENYE  ULEMAVU ( KAP) 2024 YATOLEWA.

MATOKEO YA RIPOTI YA MFUMO WA NEVA / UFAHAMU/ WATOTO WENYE ULEMAVU ( KAP) 2024 YATOLEWA.

SOS YAWEZESHA MAFUNZO YA MTAKUWWA II MKOANI IRINGA

SOS YAWEZESHA MAFUNZO YA MTAKUWWA II MKOANI IRINGA

WANANCHI NA MCHAKATO SHIRIKISHI WA KITUO CHA MALEZI MCHANA

WANANCHI NA MCHAKATO SHIRIKISHI WA KITUO CHA MALEZI MCHANA

MAAFISA USAFIRISHAJI “ BODA BODA” WAAHIDI USALAMA WA MTOTO WA KIKE

MAAFISA USAFIRISHAJI “ BODA BODA” WAAHIDI USALAMA WA MTOTO WA KIKE

SOS KUSAIDIA KUBORESHA MAZINGIRA NA USALAMA KWA MAMA MWENYE WATOTO 9 MUFINDI

SOS KUSAIDIA KUBORESHA MAZINGIRA NA USALAMA KWA MAMA MWENYE WATOTO 9 MUFINDI

VIJANA 1,651 WAPATA ELIMU AFUA ZA AFYA YA UZAZI, STADI ZA MAISHA NA UCHUMI ENDELEVU

VIJANA 1,651 WAPATA ELIMU AFUA ZA AFYA YA UZAZI, STADI ZA MAISHA NA UCHUMI ENDELEVU

UJI WA MTOTO WENYE MAKUNDI 6 YA VIRUTUBISHI

UJI WA MTOTO WENYE MAKUNDI 6 YA VIRUTUBISHI

KUUUNGUA KWA SOKO NA ATHARI KWA WATOTO WA KIUME  MTAANI

KUUUNGUA KWA SOKO NA ATHARI KWA WATOTO WA KIUME MTAANI

WANAUME 200+ NA VIKUNDI 20+ KUFIKIWA NA ELIMU YA LISHE   IRINGA -MC

WANAUME 200+ NA VIKUNDI 20+ KUFIKIWA NA ELIMU YA LISHE IRINGA -MC

NYUMA YA MKASA WA MTOTO ALIYEUAWA NA WANANCHI

NYUMA YA MKASA WA MTOTO ALIYEUAWA NA WANANCHI

KUPIKA MTORI WA  MTOTO/NDIZI MBICHI

KUPIKA MTORI WA MTOTO/NDIZI MBICHI

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]