KADI YA ALAMA KUIMARISHA MFUMO WA TAARIFA ZA MTOTO IRINGA
Автор: Makutano TV
Загружено: 2026-03-01
Просмотров: 73
Описание:
MAFINGA MJI, MUFINDI:
Ili kuhakikisha mtoto anachangamshwa na kukua vizuri katika hatua zote za ukuaji, Mkoa wa Iringa Umeanza kuwanoa maofisa wake wanaotekeleza afua za mtoto juu ya ujio wa Kadi ya alama ya Malezi na Makuzi.
Akizungumza na Makutano wiki hii, Mratibu wa Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto Mkoa Ndugu Martine Chuwa amesema
Chuwa amesema ujio wa Kadi hii ni muhimu kwa sababu, itaenda kuchochea uwajibikaji na ni nyenzo nzuri katika uwekezaji wa ralimali za afua za mtoto kama vile bajeti, mipango kitakwimu, miundombinu na utaalamu hasa wakati huu wa utekelezaji program ya MMMAM.
Disemba 4 2025, Mkurugenzi wa TECDEN Bi Mwajuma Kibwana katika uzinduzi wa mafunzo ya Kadi ya Alama kwa Maafisa Ustawi wa Jamii alisema kuwa TECDEN ina pongeza Serikali na ina furaha kuona mchakato wa kukamilika kwa kadi ya alama Nchini Tanzania .
Bi, Kibwana alitoa rai ya kuhakikisha matumizi sahihi ya utolewaji taarifa kupitia kadi hiyo kwa ngazi zote yanazingatia maslahi ya mtoto.
Kadi ya alama ya malezi na makuzi (scorecard) Tanzania ni zana itakayotumiwa na maafisa wa ustawi, elimu, na afya kufuatilia na kupima maendeleo ya watoto chini ya Miaka 8. Kadi hii inalenga kuhakikisha huduma jumuishi za Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) zinapatikana kuanzia ngazi ya familia, vituo vya afya, na madarasa ya awali.
Vipengele Muhimu:
• Kufuatilia Ukuaji: Inajumuisha hatua za kiakili, kimwili (kukaa, kutambaa, kutembea), na kijamii.
• Mafunzo: Mafunzo ya matumizi ya kadi hizi hutolewa kwa maafisa sekta mbalimbali ili kuboresha utoaji huduma.
• Wadau: TECDEN na mashirika mengine hushirikiana kuendeleza mfumo huu. #tanzaniaEDCnetwork
#childrenincrossfire
#idydcTanzania
#ECDScorecard
#MaleziCampaing
#MMMAM
#MtotoKwanza
#MtotoNiMalezi
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: