MAAFISA USAFIRISHAJI “ BODA BODA” WAAHIDI USALAMA WA MTOTO WA KIKE
Автор: Makutano TV
Загружено: 2025-09-11
Просмотров: 149
Описание:
MUFINDI
Maafisa Usafirishaji wa usafiri maarufu hapa Nchini maarufu kama “ Boda Boda “ wamekula kiapo cha ubalozi wa ulizni wa mtoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni na kuahidi usalama kwa watoto hao katika mikono yao.
Kiapo cha mabalozi hawa kimekuja kufuatia Shirika lisilo la Kiserikali la SOS Children’s Vilaage Mkoa wa Iringa kutoa mafunzo ya ulinzi na usalama wa mtoto kwa mabalozi hao wapya zaidi ya 160.
Victor Mwaipungu Meneja SOS Iringa amesema lengo la kufikia kundi hilo la usafirishaji ni kufikisha ujumbe sahihi kwa madereva wenyewe pamoja na abiria wanao wasafirisha na ulinzi shirikishi kwa jamii na kuhakikisha kila mtoto wa kike anakuwa salama dhidi ya mimba za utotoni.
Kabla ya kula kiapo Mabalozi hao wamejengewa uwezo wa elimu ya afya ya uzazi, sayansi ya malezi na ulinzi na usalama kutoka kwa wawezeshaji.
Martine Chuwa Afisa Ustawi wa Jamiii Mkoa wa Iringa, Mrakibu Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Upelelezi Kituo cha Polisi Kibao Mary Haule wamesema vitendo vya ukali na ulawiti vimekuwa vikitaja vijana katika sekta yausafirishaji kuwa kisababishi katika matukio hayo
Afisa Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu Robert Kileo Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amepongeza Shirika la SOS kwa kutoa mafunzo pamoja na jaketi na tshiŕt maalum ambazo zitasaidia kupeleka ujumbe kwa jamii
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: