🕰️ KUMBUKUMBU 📜: BARABARA ZIUNGANISHE UZALISHAJI NA MASOKO SINGIDA – RC DENDEGO
Автор: SINGIDA RS
Загружено: 2025-12-24
Просмотров: 40
Описание:
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, alifungua kikao cha 48 cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Singida na kuweka mwelekeo mpya wa maendeleo ya miundombinu. RC Dendego alieleza mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita katika ujenzi na ukarabati wa barabara, madaraja, makalavati na vivuko, huku akisisitiza ulinzi wa miundombinu, uwajibikaji wa watendaji na ubunifu katika utekelezaji wa miradi.
Lengo kuu: kuhakikisha Singida ina mtandao imara wa barabara unaounganisha uzalishaji na masoko, kukuza biashara na huduma, na kuiandaa Singida kuwa jiji la kisasa lenye hadhi ya kimataifa – Dubai na Singapore ya Tanzania.
14 Januari 2025
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, aliutaka Mkoa wa Singida kutumia fursa ya uwekezaji mkubwa wa Serikali ya Awamu ya Sita katika miundombinu ya barabara kuhakikisha maeneo yote, hususan ya vijijini na uzalishaji, yanafikika wakati wote, huku akisisitiza ulinzi wa miundombinu, uwajibikaji wa watendaji na ubunifu katika utekelezaji wa miradi ili kuufanya Singida kuwa kitovu cha biashara na huduma chenye hadhi ya kimataifa.
Mhe. Dendego alitoa kauli hiyo wakati akifungua rasmi kikao cha 48 cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Singida, 14 Januari 2025 ,akitoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipatia Singida fedha nyingi za barabara. Alisema kwa mwaka wa fedha uliopita, Mkoa uliidhinishiwa zaidi ya Tsh bilioni 49.4, huku mwaka wa fedha 2024/2025 ukiidhinishiwa Tsh bilioni 48.2 kupitia TANROADS na TARURA, fedha zinazolenga kuboresha barabara, madaraja, makalavati na vivuko.
Alieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu na miezi kadhaa ya Serikali ya Awamu ya Sita, Singida imepiga hatua kubwa kwa kuongeza kilometa za barabara, barabara za changarawe, pamoja na kukamilisha ujenzi wa madaraja makubwa na madogo, makalavati na vivuko, hali iliyoongeza upitikanaji wa barabara kwa mwaka mzima hadi zaidi ya asilimia 82. Mhe. Dendego alisema mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa wa fedha na usimamizi wa karibu wa miradi.
Katika maelekezo yake, Mkuu wa Mkoa alisitiza kuwa wajibu wa kwanza wa viongozi na wananchi ni kulinda miundombinu hiyo, akionya kuwa uharibifu unaotokana na uzembe au vitendo vya makusudi kama kung’oa vyuma kwenye madaraja, kumwaga mafuta barabarani au ajali za kizembe, hatua kali zichukuliwe bila kusita. Aidha, amewaagiza watendaji kufanya matengenezo mara moja panapotokea uharibifu wowote ili barabara ziendelee kupitika wakati wote.
Akihitimisha, Mhe. Dendego ameeleza kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kuhakikisha mtandao wa barabara unaunganisha maeneo ya uzalishaji na masoko ili kukuza biashara na huduma, sambamba na maono ya kuifanya Singida kuwa jiji la kisasa. Amewataka wataalamu na watendaji kuwa wabunifu, kuzingatia thamani ya fedha na kujenga barabara zinazokidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye, huku miundo ya barabara ikielekezwa katika viwango vya kimataifa kama vya Dubai na Singapore, ili kuiandaa Singida ya kesho.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: