🔴 PRESS: WADAIWA MADENI YA TUMBAKU SINGIDA WASHIKILIWA
Автор: SINGIDA RS
Загружено: 2025-12-18
Просмотров: 175
Описание:
Mkoa wa Singida unaendelea kuchukua hatua madhubuti kufuatilia malipo ya madeni ya wakulima wa tumbaku kwa msimu wa kilimo 2024/2025, kufuatia ucheleweshaji wa malipo kwa zaidi ya miezi minne unaohusisha makampuni matatu ya ununuzi wa tumbaku.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, Katibu Tawala Msaidizi wa Huduma za Uzalishaji na Uchumi Mkoa wa Singida, Bw. Stenslaus Beatus Choaj, amesema ucheleweshaji huo ni ukiukwaji wa mikataba kati ya vyama vya wakulima na makampuni husika.
Amesema Mkoa umeanza kuwashikilia wawakilishi wa makampuni mawili ya Biexen Company Ltd na Magefa Growers Ltd kwa kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, huku kampuni ya Famous Rock Private Ltd ikikaidi kabisa wito wa kufika au kutuma mwakilishi wake katika vikao vilivyoitishwa.
Hatua hizi zimelenga kulinda haki za wakulima na kuhakikisha wanalipwa fedha zao kwa mujibu wa makubaliano.
Kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Tumbaku Tanzania, katika msimu wa kilimo 2024/2025 jumla ya kilo 1,742,651.33 za tumbaku zimenunuliwa mkoani Singida zenye thamani ya Dola za Marekani 4,188,969.81. Kati ya fedha hizo, Dola 3,384,158.78 sawa na asilimia 80.79 zimeshalipwa, huku Dola 804,811.03 sawa na asilimia 19.11 bado ni madeni. Madeni hayo yanadaiwa na Magefa Growers Ltd (USD 465,211.19), Biexen Company Ltd (USD 297,355.18) na Famous Rock Private Ltd (USD 42,344.66).
Bw. Choaj amewahakikishia wakulima kuwa Serikali kupitia Bodi ya Tumbaku kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inaendelea kuchukua hatua za haraka ikiwemo kusimamia mauzo ya tumbaku za makampuni husika ili fedha zipatikane kwa ajili ya kuwalipa wakulima.
Amesisitiza kuwa Mkoa wa Singida hautavumilia kampuni yoyote inayokiuka mikataba na kuchelewesha malipo ya wakulima, akizitaka kampuni zote za ununuzi wa mazao ya kilimo kuwa waaminifu na kuwaheshimu wakulima.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: