DKT NCHEMBA: WANANCHI WA KIPUNGUNI KULIPWA FIDIA
Автор: Hazina TV - Wizara ya Fedha
Загружено: 2024-04-08
Просмотров: 797
Описание:
Serikali imesema kuwa itaanza kufanya malipo ya fidia kwa wananchi wa Kipunguni waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam ambao madai yao yamehakikiwa na hayana vikwazo vyovyote.
Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu, aliyetaka kujua wakati ambao Serikali itawalipa fidia wananchi wa Kipunguni waliopisha ujenzi wa Uwanja wa Ndenge wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: